Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, September 16, 2012

Siku Maalum ya Mtanzania Imefana Ndani ya Ubalozi wa Tanzania Washington DC

Sunday, September 16, 2012
Ubalozi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Washington D.C Jana umeandaa Maonyesho ya kwanza ya aina yake ya siku maalum ya Mtanzania kuonyesha Utamaduni wake ambapo watu wengi walihudhuria huko kwenye Jengo la ubalozi kuangalia bidhaa mbalimbali za kitanzania.


Ikiwa ni siku maalum ya Mtanzania ilotolewa wito na Mhe. Mwanaidi Maajar, Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico,  Siku ya Ijumaa, Sept. 14, 2012,  Wananchi wengi wa Kitanzania na hapa Marekani walikuweko kuangalia maonyesho na kununua bidhaa ikiwemo Mavazi ya kanga batiki,vitenge, shanga, mapishi ya vyakula mbali mbali vya kinyumbani,pamoja  na vivutio vya utalii kutoka kwa wajasirimali

Wengi walionyesha kufurahishwa na Siku hii maalum ya mtanzania kwani ilikuwa na vivutio vingi hasa mambo ya watanzania kuwa ni watu maalum kabisa na fursa za kitalii za kuweza kuwekeza huko Tanzania pia taasisi za kudumisha Lugha ya Kiswahili na ngoma za utamaduni.

Maonyesho hayo yalifanyika katika eneo la Ubalozi wa Tanzania Jijini Washington DC -picha ya juu na chini hapa


Jengo la Ubalozi wa Tanzania  katika siku Maalum ya Mtanzania iliofanyika siku ya Jumamosi  Sept, 15, 2012

 Katibu wa Jumuia ya waTanzania DMV Bwna. Amos Cherehani akiwa na muweka hazina wakikaribisha wageni ndani ya jengo!

 Susan Malima Mfaya biashara wa mapambo ya kiasili

Mteja akiangalia bidhaa za Kwetu Fashion Desig kwa manunuzi

Kwetu Fashion Desig Missy Temeke  alivaa vazi la kitamaduni, akiwa na wateja wake njee ya jengo la Balozi waTanzania siku ya Tanzania Day

Mjasirimali Haji S. Abdulla wa usafirishaji wa mizigo kutoka Marekani kwenda Tanzania wa Rodger's Exports

Mhe. Mwanaidi Maajar, Balozi wa Tanzania Nchini Marekani na Mexico alivaa vazi la kitenge akiwakaribisha wageni walikwa ndania ya Tanzania House, kwa maonyesho ya kitamatuni. pamoja na Watoto wa Mhe. Leticia M Nyerere, Helena Maria Nyerere na Julia Nyerere.

Cheif wa swahilivilla  akiangalia bidhaa mbali mbali za wajasirimali  





















Maelezo na picha zote na swahilivilla 

No comments :

Post a Comment