Wazanzibari waishio Canada ambao karibuni waliunda association yao inayoitwa Zanzibar-Canadian Diaspora Association (ZACADIA) na ambayo ime-register a charity foundation ijulikanayo kama ZACADIA Foundation imeanzisha mradi wa kuwasaidia watoto maskini wa Unguja na Pemba.
Soma zaidi hapa chini.
ZANZIBAR-CANADIAN DIASPORA ASSOCIATION (ZACADIA)

ZACADIA
Muandishi: Hapa Pangu
Sunday, September, 2012.
Kwa niaba ya Katibu wa ZACADIA (Zanzibar-Canadian Diaspora Association) ya Canada, tunawashukuru wale waliojitokeza kuisaida ZACADIA kutengeneza LOGO mpya. Ni matumaini yetu kwamba LOGO yetu mpya itafikishwa na wale waliojitokeza hivi karibuni, na mara tu ikipatikana itatangazwa katika Mzalendo.net kwa utambulisho.
Wakati huo huo, ZACADIA inawataarifu Wazanzibari wote wanaoishi nje na ndani ya nchi, kuwa imebuni mradi wa kijamii kwa ajili ya kuwasaida watoto mayatima na masikini ambao wazee wao au walezi wao wako katika hali duni sana ya kimasiha na ambayo inawapelekea kushughulikia zaidi maisha yao kuliko kuwashajiisha watoto wao kwenda skuli na hatimaye watoto hao kuishia kwenda kutega ndege na kucheza badala ya kwenda skuli au kutafuta kazi ambazo si kiasi chao au bila kufikia wakati wao wa kufanya kazi.
Mradi huu utakuwa ni sawa na ile miradi inayofanywa na taasisi nyengine za kimataifa, za kutafuta wadhamini (SPONSORS) wa kuwadhamini watoto kwa dola 30 kwa mtot mmoja kwa mwezi, mapka pale mtoto huyo amalize sekondari, ili mtoto huyo aweze kupatiwa maisha bora na wazazi wake kusaidiwa kwa kiasi fulani kwa njia isiyo ya moja kwa moja kifedha, ili aweze kujali kumshawishi mtoto wake aende skuli na huku akihudumiwa na ZACADIA kutokana na wadhamini hao ambao watalengwa zaidi Wazanzibari walioko nje na pia kutafuta fedha kwa njia nyengine kama vile Fundraising na misaada kutoka Taasisi nyengine za kibinaadamu nchi za nje ili kuongezea katika dola 30 za mdhamini.
Jumuia nyingi duniani kama vile World Vision, Children Funds, Canadian Christian Child Fund na nyengine zinasaidia watoto wa nchi mbali mbali bila kufika misaada ya aina hii katika visiwa vya Zanzibar, na ambapo misaada hiyo huishia Tanganyika tu.
Ni matumaini ya ZACADIA kwamba Wazanzibari wengi watajitokeza pamoja na marafiki zao wasio na asili ya Zanzibar katika kuufanikisha mradi huu wenye lengo la kuwaondoshea watoto masikini na mayatima tatizo la vifaa vya skuli, uniform, usafiri, chakula bora na uangalizi wa kiafya.
Maelezo zaidi yatatolewa mara tu web site itakapomalizika kujemgwa pamoja na LOGO yetu mpya.
Tunatanguliza shukrani za dhati kwenu nyote.
Source: ZACADIA
No comments :
Post a Comment