MAHAKAMANI VUGA
22-11-2012
NA Masoud Ali
VIONGOZI WA UAMSHO AMBAO KWA SASA TAYARI WAMESHAKAA RUMANDE KWA MUDA WA MWEZI MMOJA WAMEFIKISHWA TENA KATIKA MHAKAMA KUU YA VUGA ASUBUHI YA LEO KWA LENGO LA KUPELEKA MADAI YAO KATIKA MAHAKAMA KUU DHIDI YA UONEVU WANAOFANYIWA WANAPOKUWA RUMANDE,.
VIONGOZI HAO WALIFIKISHWA HAPO SAA TATU ASUBUHI AMBAPO KABLA YA HAPO MAKACHERO WA ASKARI POLISI WALIWAHI KUFIKA ILI KUWEZA KUWAZUIA WANANCHI WASISOGEE KATIKA ENEO HILO IKIWA NI AGIZO MAALUM KUTOKA KWA VYOMBO VYA ULINZI KUTOKANA NA KITENDO KISICHOTARAJIWA ALICHOKIFANYA SHEHE FARIDI CHA KUWAULIZA WANANCHI KUHUSU MUUNGANO NA WAO KUJIBU KWA SAUTI MOJA KWAMBA HAWAUTAKI WAKATI WALIPOKUA WAKITOKA KATIKA KESI ILIOENDESHWA TAREHE 20-11-2012 MAHAKAMANI HAPO VUGA.
MADAI HAYO YALIWASILISHWA KWA DPP RAYA MSELEM NA RAMADHAN NASIBU CHINI YA JAJI MKUSA ISAC SEPETU. AMBAPO DPP HAO WAMEOMBA WAPATIWE SIKU KUMI NA NNE KUWEZA KUIPITIA SAMAS YA KESI HIYO KWA KUWA HAWAKUTAARIFIWA MAPEMA.
NA KWA UPANDE WA MAWAKILI WA WASHTAKIWA HAO ABDALLAH JUMA NA SALUM TAWFIQ WAMESEMA HAWAPINGANI NA MAOMBI YA DPP HAO KWA KUWA WANAHAKI YA KISHERIA KUDAI MUDA LAKINI WAMESEMA MUDA WALIOTOWA NI MKUBWA HIVYO WAMEIOMBA MAHAKAMA WAUPUNGUZE MUDA ILI KUWEZA KUJUA KAMA KUNA ULAZIMA WA KUONGEZA MADAI MENGINE AU HAYO WALIOYATOWA YANATOSHA.
AIDHA WAMEIOMBA MAHAKAMA KULITILIA MKAZO SUALA KUPUNGUZIWA MUDA KWA KUWA BADO WATEJA WAO WAPO RUMANDE HIVYO KADRI WANAVYOENDELEA KUKAA NDIVO UONEVU UNAVYONGEZEKA.
BAADA YA MVUTANO MKUBWA KATI YA UPANDE WA DPP NA MAWAKILI HAO JAJI ISAC SEPETU AMESEMA SHERIA YA GEREZA NO 2 YA MWAKA 2007 ITEKELEZWE, NA BAADAE KUAMUA KUWAPA WIKI MOJA KUWEZA KUYAPITIA NA BAADAE KURUDI TAREHE 29-11-2012 KWA AJILI YA KUSIKILIZWA NA KUTOLEWA UFAFANUZI WA MADAI HAYO…
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment