Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, November 23, 2012

Wapendekeza nafasi ya Makamu wa Rais ifutwe wakazi wa Dar

Written by   //  23/11/2012  //  Habari  //  2 Comments

Wapendekeza nafasi ya Makamu wa Rais ifutwe

NA ELIZABETH ZAYA
23rd November 2012

Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wamependekeza nafasi ya Makamu wa Rais iondolewe na badala yake msaidizi wa Rais awe ni Waziri Mkuu.
Wakitoa maoni ya kuundwa kwa katiba mpya, jana katika viwanja vya Gonga, wilayani Ilala jijini Dar es Salaam, walisema Makamu wa Rais hana majukumu mazito ya kufanya.
“Hatuoni umuhimu wa kuwepo kwa nafasi ya makamu wa Rais kwa sababu hakuna majukumu mazito anayoyatenda hivyo ni vyema msaidizi wa Rais akawa ni Waziri Mkuu,” alisema Ndaji Saimon nakuongeza:
“Ikitokea Rais hayupo au Waziri Mkuu nae hayupo nafasi hiyo itakaimiwa na Spika au Jaji Mkuu,” alisema.
Sadick Masawe, alisema kama Serikali inapaswa kuafikiana na maoni ya kufutwa nafasi ya Makamu wa Rais.
Aidha, wananchi hao walipendekeza kuwapo kwa kikomo cha ubunge ili kuwapa nafasi watu wengine wenye sifa na uwezo wa kuongoza.
Walisema kuwa wabunge wanapaswa kutumikia nafasi hiyo kuanzia miaka mitano hadi 10 na baada ya hapo waziachie nafasi hizo kwa watu wengine.
“Upo uwezekano wa kuziba nafasi za watu wengine, kiongozi ataendelea kushikilia madaraka kwa muda mrefu na hivyo kuwakosesha fursa hiyo watu wengine,” alisema Hassan Said.
Kuhusu elimu walipendekeza elimu ya kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne itolewe bure na iboreshwe zaidi.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment