dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 28, 2012

Japan Kugharamia Kiwanja Pemba

Written by   //  28/11/2012 

Na Ali Issa-Maelezo Zanzíbar
Jumla ya Shilingi milioni 200 za kitanzania zinatarajiwa kutolewa na Serikali ya Japan kwa ajili ya kugharimia Uwanja wa michezo mbalimbali utakaojengwa Kisiwani Pemba.
Balozi wa Japan nchini Tanzania Takumi Shimojo ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk ofisini kwake leo Kikwajuni mjini Zanzíbar.
Amesema Serikali ya Japani inakusudia kujenga uwanja wa Michezo kisiwani Pemba mara tu nchi hiyo itakapoidhinisha kuanza kwa kazi hiyo hapo mwakani .
Amefahamisha kuwa Uwanja huo utakaojumuisha michezo ya Judo, Karatee,Mpira wa Kikapu, Tebuli tenis na michezo mingine utajengwa ikiwa ni njia ya kuimarisha mahusiano mema kati ya Japan na Zanzíbar .
Balozi Takumi amefahamisha kuwa ingawa Mkandarasi wa kiwanja hicho kinachotarajiwa kujengwa mwakani mwezi wa Juni na Julia hajatangazwa lakini mipango yote imeshakamilika .
Nae waziri Said Ali Mbarouk alimshukuru Balozi huyo kwa msaada wa ujenzi huo na kusema kuwa kitendo hicho ni cha kupongezwa kwa Serikali ya Japani kuifanyia Zanzíbar kiwanja hicho hasa kwa Pemba ili wananchi wa huko wafarijike na Kiwanja hicho kama ndugu zao wa Unguja.
Amesema jitihada hizo za Japani ni zakutia moyo kwani zitasaidia Wanamichezo wa Pemba kujenga miili yao na kutunza afya zao sambamba na kukitumia kiwanja hicho kama mtaji wa kujiandaa kwa mashindano ya kitaifa na kimataifa.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment