Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Wednesday, November 28, 2012

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR YALALAMIKA

MHE. ALI JUMA SHAMUHUNA 
Written by Harith // 27/11/2012.
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR IMEILAUMU WIZARA YA ELIMU YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA MADAI YA KUTOISHIRIKISHA IPASAVYO WAKATI INAPOFANYA MABADILIKO HASUSAN YANAYOHUSIANA NA MITIHANI YA TAIFA.

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR NDUGU ALI JUMA SHAMUHUNA AMETOA MALALAMIKO HAYO MBELE YA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIF HAMAD HUKO MAKAO MAKUU YA WIZARA HIYO MAZIZINI, IKIWA NI SIKU YA KWANZA YA ZIARA YA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS KATIKA SEKTA YA ELIMU.

WAZIRI SHAMUHUNA AMEFAHAMISHA KUWA WIZARA YA ELIMU TANZANIA KUPITIA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA, MARA NYINGI IMEKUWA IKAFANYA MAAMUZI BILA YA KUISHIRIKISHA WIZARA YA ELIMU ZANZIBAR, JAMBO AMBALO LINAWAPA UGUMU WA KUETEKELEZA MIPANGO YAO IKIWA NI PAMOJA NA KUWAANDAA WANAFUNZI KUWEZA KUYAFAHAMU MABADILIKO YANAYOFANYWA NA BARAZA LA MITIHANI.

AMETOA MFANO WA MAAMUZI YALIYOFANYWA HIVI KARIBUNI NA BARAZA LA MITIHANI YA KUWAZUIA BAADHI YA WANAFUNZI KUTOFANYA MITIHANI YAO YA KIDATO CHA SITA MWEZI FEBRUARI MWAKANI KWA MADAI YA KUTOTIMIZA MASHARTI YA KUFANYA MTIHANI HUO,AMBAPO AMESEMA WIZARA YAKE HAIKUPEWA TAARIFA MAPEMA KUHUSU MASHARTI MAPYA YA SIFA ZA KUFANYA MTIHANI WA KIDATO CHA SITA.
AMESEMA KUWA WIZARA HIYO IMEKUWA IKIKWEPA KUIARIFU WIZARA YAKE KUHUSU MABADILIKO YANAYOFANYWA NA BARAZA LA MITIHANI LA TAIFA, NA BADALA YAKE IMEKUWA IKIZIARIFU SKULI BINAFSI, JAMBO AMBALO NI KINYUME NA UTARATIBU.

AMESEMA KUWA HALI HIYO IMEKUWA IKICHANGIA KUTOA MATOKEO MABAYA KWA WANAFUNZI WA ZANZIBAR KUTOKANA NA KUTOARIFIWA MAPEMA MABADILIKO YANAYOFANYWA IKIWA NI PAMOJA NA KUBADILIKA KWA RATIBA ZA MITIHANI PAMOJA NA MUONGOZO WA KUFUNDISHIA KWA BAADHI YA MASOMO.

AKIZUNGUMZIA SUALA HILO MAKAMU WA KWANZA WA RAIS AMEZISHAURI WIZARA HIZO KUKAA PAMOJA NA KUJADILIANA KUHUSU HATUA BORA ZA KUCHUKULIWA KATIKA KUONDOSHA TOFAUTI HIZO, NA KUELEZEA HAJA YA KUWEPO KWA MASHIRIKIANO YA KARIBU KATI YA WIZARA HIZO MBILI.

BAADA YA KUPOKEA TAARIFA YA WIZARA HIYO ILIYOWASILISHWA NA NAIBU KATIBU MKUU BW. ABDALLA MZEE, MAALIM SEIF ALIHOJI UHABA WA MADARASA YA KUSOMEA PAMOJA NA VIKALIO KATIKA SKULI MBALI MBALI UNGUJA NA PEMBA.

AIDHA MAALIM SEIF AMEELEZEA HAJA YA KUREJESHWA KWA HUDUMA ZA DAKHALIA ILI KUWAONDOSHEA USUMBUFU WANAFUNZI WANAOTOKA MAENEO YA MBALI, HOJA AMBAYO IMEUNGWA MKONO NA UONGOZI WA WIZARA HIYO KWAMBA WAMELIFIKIRIA KWA MUDA MREFU SUALA HILO LICHA YA KUKABILIWA NA UFINYU WA BAJETI.

HATA HIVYO KATIBU MKUU WA WIZARA HIYO BI. MWANAIDI SALEH AMESEMA WIZARA HIYO INA DHAMIRA YA KUREJESHA HUDUMA HIYO KWA WANAFUNZI WAKATI WOWOTE HALI YA BAJETI ITAKAPORUHUSU.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment