Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 5, 2013

ZANZIBAR: Failure ya Mwanzo kwa Dr Shein Katika Mwaka 2013

Written by   //  04/01/2013
Dr Shein panua masikio usikie wengine mawazo ya wengine ili uweze kufanikiwa uongozi wako
-Apangiwa kufungua mradi “butu”
- Afanya uteuzi wenye utata wa hali ya juu
Wengi tunafahamu dunia inapopitia huku nchi nyingi tukiziona zikijikita na kujiingiza kwenye hicho kinachoitwa “TEKNOLOJIA. Inafahaimaka fika kuwa Teknolojia ni uwanja mpana, hapa tutazungumza teknolojia moja ambayo ni E-GOVERNMENT.
Kama ilivyotangazwa kwenye ratiba ya sherehe za mapinduzi, hiyo kesho kutakuwa na ufunguzi wa mradi wa E-GOVERNMENT hapo kwenye ofisi ya mradi huo. Imesemwa kuwa Dr Shein atafanya ufunguzi huo wakati wa jioni.
Dr Shein kwenye mradi huu kauziwa “paka kwenye gunia”. Mradi umegharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi. Sijuwi ni kitu gani Dr Shein anakwenda kukifungua hiyo kesho hapo Mazizini. Hivi Dr Shein anajuwa maana ya E-Government?
Dr Shein E-Government ni zaidi na hicho unachokwenda kukishuhudia kesho. Unachotakiwa kukifahamu ni kuwa unapofunga E-Government ni kwamba chochote unachotaka kukijuwa kilichoko Wizara Fedha, technolojia ikuruhusu kufanya hivyo.
Dr Shein E-Government sio kuunganishwa na kuzungumza kwa video conference kwa yule aliye Pemba na Unguja. Hivyo ni kuijaribu “Fibre Cable”. Wala hatuwezi kuiita E-Government.
Dr Shein hiyo failure ya mwanzo unaianza kwa mwaka huu mpya. Unapaswa kupanua masikio na kusikiliza wengine wanasema nini.
Kosa jengine lililofanyika ni kwa ule uteuzi wa Mkurugenzi wa ICT katika Wizara ya Utumishi na Utawala Bora. Uteuzi huu umeleta utata mkubwa kwani sector hii imeundwa ndani ya wizara tatu tofauti. Ndani ya Wizara ya Elimu, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano na sasa iko kwenye Wizara ya Utumishi na Utawala Bora hivyo kulenga mgongano mkubwa kwa wakurugenzi hao watatu.
Hivi karibuni Dr Shein alifanya uteuzi wa Bw Shaaban Choum kuwa Mkurugenzi wa ICT ndani ya Wizara ya Utumishi na Utawala Bora, hivyo kuleta mparaganyo mkubwa kiasi cha hata wakurugenzi wengine kususia uteuzi huo na kuahidi kutotoa ushirikiano na mkurugenzi huyu.
Taarifa zaidi inasema kuwa hata uwezo wake ni mdogo sana huku akihusishwa na “mascandal” ya ubadhirfu na mamilioni ya fedha.
Ningemshauru Dr Shein amkatae paka hadi atoke nje. Asifungue mradi huu hadi ifahamike fika kwamba mradi umekamilika. Ukifuatilia muundo wa serikali yake hauna tofauti na Serikali ya Mungano, hivi kwanini Dr Shein hakuiga kule Bara walivyofanya mradi wao wa E-Government. Wao wameita “Agency” kabisa na hawakutaka kuutia kwapani mradi huu. Faida yake mradi umekamilika na unafanya kazi yake kama ilivyotarajiwa.
Dr Shein, umeanza mwaka mpya na kufeli kiana hii. Kumbuka unakaribia nusu ya muhula wa uongozi wako. Ipo haja ya kupata ushauri stahiki kwa wataalam wanaofahamu kwa kina juu ya mradi huu. 20milion  USD ni fedha nyingi sana, hazilingani na matumizi ya gharama na utekelezaji wa mradi huu.
Bado hujachelewa, ukiwa na nia safi unaweza kuufanya mradi huu kufanikiwa.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment