Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, January 18, 2013

ZANZIBAR: Mswada wa ruzuku vyama vya siasa wapita bila kupingwa


 

DSC06898
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilshi wameupitisha kwa sauti moja mswada wa marekebisho sheria ya ruzuku kwa vyama vya siasa nambari 6 ya mwaka 1997.
Mswada huo pamoja na mambo mengine lengo lake ni kuondoa kasoro zilizopo katika sheria hiyo ili iweze kwenda sambamba na hali halisi ilivyo ya ruzuku kwa vyama vya siasa pamoja kuvipa uwezo vyama vya siasa ili viweze kuendeleza demokrasia nchini.
Akifanya majumuisho ya mswada huo Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba suala la ruzuku kwa vyama vya siasa limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu na hivyo serikali imeamua kuwasilisha mswada huo ili kuondosha manunguniko hayo.
Aboud alisema sheria ya ruzuku kwa vyama vya siasa ipo tangu mwaka 1997 lakini ilishindikana kutekelezwa kwa sababu Serikali haikuwa na mapato ya kutosha ya kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa.
“Tumewasilisha marekebisho ya mswada wa ruzuku kwa vyama vya siasa kwa lengo la kuhakikisha kwamba vyama hivyo vinatekeleza dhana ya demokrasia na utawala bora kwa ajili ya  kuendesha shunguli za kisiasa” alisema Aboud.
Katika marekebisho mapya yaliyowasilishwa mbele ya wajumbe wa baraza la wawakilishi, vyama vya siasa vitapata ruzuku si zaidi ya asilimia mia moja.
Katika mchanganuo huo, kwa chama kitakachoshinda kiti cha urais kitapata mgao asilimia 20 %,wakati mgawanyo kwa vyama vitakavyopata majimbo ya uwakilishi utakuwa asilimia 50 %na majimbo ya udiwani katika serikali za mitaa ni asilimia 30%.
Alisema marekebisho ya sheria hiyo yataongeza ushindani kwa vyama vya siasa zaidi katika kipindi cha uchaguzi mkuu lakini chini ya sheria hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza demokrasia kwa kuwa kutakuwa na ruzuku kwa vyama hivyo.
Alisema kuwa  tokea kupitishwa kwa sheria hiyo mwaka 1997 utekelezaji wake umeshindwa kutekelezeka kutokana na sababu mbili kuu ambapo kifungu cha tatu cha sheria hiyo kinasema kuwa ruzuku inayotolewa na Serikali isipunguwe asilimia moja ya bajeti ya kawaida kiwango ambacho ni kikubwa hasa ikizingatiwa na changamoto za kiuchumi, kijamii na kisiasa ambazo Serikali inapaswa kukabiliana nazo.
Sababu nyengine ni mgawanyo wa ruzuku hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha sheria ambacho kinahimiza asilimia 50 ya ruzuku kwa chama
kilichopata kiti cha urais, aslimia 30, kwa mujibu wa uwiyano wa viti
vya majimbo ya wawakilishi na asilimia 20 kwa mujibu wa uwiyano wa
viti vya wadi, mgawanyo ambao umekuwa ukilalamikiwa kuwa hauzingatii mustakabali wa vyama vya kisiasa na kiuendeshaji.
Hivyo amependekeza kifungu cha tatu kifanyiwe marekebisho kwa kuwekwa kima cha ruzuku kisichozidi aslimia moja ya bajeti ya kawaida ya kila mwaka ya Serikali, kifungu cha tano kiwekwe mgao mpya wa asilimia 20 ya ruzuku iende kwa chama kilichoshinda kiti cha urais, asilimia 50 ya ruzuku itagawiwa kwa uwiyano wa viti vya majimbo na asilimia30 itagawiwa kwa uwiyano wa viti udiwani.
Awali wakichangia katika mswada huo wajumbe wa baraza hilo walifurahishwa kuletewa mswada huo ambao wamesema utaondosha ukata katika vyama vya siasa lakini pia utasaidia kuvihuisha vyama ambavyo vilikuwa na matatizo ya kifedha na kuondosha kuomba fedha kwa wafadhili jambo ambalo linaweza kuweka masharti kwa wenye kutoa misaada kwa vyama hivyo.
Tangu kupitishwa kwa sheria hiyo katika mwaka 1997 katika kipindi cha utawala wa rasi mstaafu Dk.Salmin Amour Juma, sheria hiyo haikuweza kufanya kazi na vyama vya siasa ikiwemo CCM na CUF kushindwa kupata ruzuku.
MWISHO
 
  Uharibifu wa mazingira hufanya na binaadamu
IMEELEZWA kwamba kupungua kwa uwezo wa vianzio vya maji katika maeneo ya Chaani, Gamba na Moga Mkoa wa Kaskazini Unguja kumetokana uharibifu na kazi tofauti zinazofanywa na binadamu katika maeneo hayo.
Naibu Waziri wa Kilimo na Maliasili, Mtumwa Kheri
Mbarouk alipokuwa akijibu suali la mwakilishi wa jimbo la Chaani,.
Ussi Jecha Simai huko katika kikao cha baraza la wawakilishi
kinachoendelea Mjini Zanzibar.
Alisema kuwa hatua hiyo husababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kupotea kwa uoto wa asili hasa ukataji mkubwa wa miti kwa ajili ya
kujipatia nishati ya kuni pamoja na matumizi ya ardhi.
Hivyo amesema kuwa katika kuhakikisha hali hiyo inapotea wizara yake
imeielimisha jamii juu ya changamoto hiyo na hivyo kila mmoja
kushiriki kuzuia uharibifu huo.
Aidha alisema kuwa uelimishaji huo umelenga kupandwa miti katika
maeneo yote ya vianzio vya maji na kuendelezwa, pamoja na vianzio
mbadala vya maji kwa kuchimwa visima vidogo na vikubwa katika
kutekeleza mpango wa Umwagiliaji maji.
Hata hivyo amesema kwamba wiazara imeaandaa mpango wa kuendeleza maeneo ya kilimo yawe ya umwagiliaji maji na hivi sasa inaada program na miradi midogo midogo kwa ajili kupata fedha za utekelezaji.
Katika sauli lake mwakilishi Simai alitaka kujua Serikali ina mpango
gani wa kuwapatia wakulima vyanzo vya maji mbadala kwa ajili ya mazao
yao.
MWISHO
Wizara haina nia ya kuweka matabaka katika utoaji wa mikopo
NAIBU waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar  Zahra Ali Hamad amesema kuwa wizara yake haina nia ya kuweka matabaka katika utoaji wa mikopo ya elimu ya juu.
Kauli hiyo ameitoa leo katika kikao cha baraza la wawakilishi kilichoanza leo wakati akijibu suali la nyongeza la mwakilishi wa jimbo la Chake Chake, Omar Ali Shehe ambae alitaka Serikali inampangogani wa kuweza kuwaandalia wanafunzi kuhusu utoaji wa mikopo ili wote waweze kukosa au kupata ili kuwa ni viwango sawa vya elimu kuliko kutoa kwa matabaka.
Omar amesema kuwa kutoa mikopo hiyo kwa matabaka kunakofanywa na bodi ya mikopo ni kwenda kinyume na malengo ya Mapinduzi ya Zanzibar ambayo ni kutoa elimu kwa wote.
Zahra alisema kuwa hawajmbagua mtu katika utoaji wa mikopo bali ukosefu wa fedha ndio unaofanya baadhi ya wanafunzi kukosa kupatiwa mikopo hiyo.
Nae mwakilishi wa viti maalumu, Kazija Khamis Kona alitaka kujua sababu zilizopelekea uwalazimisha wazazi na walezi wa wanafunzi kulipia elimu wakati baada ya kupatikana uhuru rais wa awamu ya kwanza wa  Zanzibar marehemu Mzee Abeid Karume alishatangaza elimu bure.
Akijibu suali hilo Zahra amesema kuwa kiwango cha fedha kinachotolewa na wazazi wa wanafunzi ni mchango na sio kama wanasoma kwa malipo, kiwango ambacho hakifikii hata asilimia ziro ya mahitaji ya elimu yenyewe.
Mapema akijibu suali la msingi alisema kuwa Serikali inatambuwa kiwango cha fedha cha mkopo kinachotolewa hakitoshelezi mahitaji yote ya wanafunzi na mzazi au mlezi anawajibu wa kugharamia mahitaji mengine ya mwanafunzi.
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema bodi ya mikopo ya Zanzibar  ipo katika mikakati ya kutafuta  vyanzo zaidi vya mapato kwa ajili ya kuweza kutekeleza majukumu yake ikiwemo kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zahra Hamad wakati alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi wa jimbo la KIKWAJUNI  Mahmoud Mohamed Mussa aliyetaka kujuwa bodi ya mikopo kwa nini imeshindwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu nchini.
Akijibu swali hilo Zahra alisema uchache wa fedha zinazotolewa kutoka hazina kwa ajili ya bodi ya mikopo kutoa mikopo ya elimu kwa wanafunzi ni kikwazo kikubwa.
Akifafanua alisema katika mwaka 2011-2012 bodi ya mikopo ilipatiwa jumla ya sh.Bilioni 4,wakati maombi ya wanafunzi wanaohitaji mikopo yalikuwa 1,850.
Hata hivyo Zahra alisema wanafunzi waliopata mikopo hiyo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu ni 209 ikiwa sawa na asilimia 11.3.
Alisema bajeti ya Bodi ya mikopo iliyotengwa kwa mwaka wa fedha 2012-2013 ni sh.Bilioni 8 wakati maombi ya mahitaji ya wanafunzi ni 320.
Hata hivyo alisema bodi ya mikopo ilifanikiwa kuwapatia mikopo wanafunzi wapatao 800 ikiwa kinyume na mahitaji ya wanafunzi.
Alivitaja viwango vinavyotolewa mikopo kwa wanafunzi wenye mahitaji hayo vinatofautiana na masomo yenyewe.
Kwa mfano alisema masomo ya sanaa viwango vya fedha ni kidogo tofauti na masomo ya sayansi,huku wanafunzi wanaosoma katika vyuo vya elimu ya juu viliopo Zanzibar hupewa kiasi cha sh.Milioni 2.
Alisema wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu viliopo Tanzania Bara hupatiwa sh.Milioni tatu na bodi ya mikopo wakati wanafunzi wanaosoma katika Vyuo vikuu vya nje ikiwemo China hupewa kiwango cha sh.Milioni 12.
‘Viwango vya fedha wanavyopatiwa wanafunzi wetu na bodi ya mikopo ni kidogo kutokana na bajeti halisi wanayotengewa na Serikali’alisema.
Alisema kwa sasa bodi ipo katika mchakato wa kufanya mapitio ya viwango vya fedha zinazotolewa kwa wanafunzi wanaopata mikopo pamoja na kuangalia vyanzo vya kuongeza mapato zaidi.
‘Hiyo ndiyo mikakati ya bodi ya mikopo ya elimu ya juu…..kufanya mapitia ya sheria ya viwango vya mikopo lakini pia kuangalia vyanzo vya kuongeza mapato zaidi’alisema.
Wanafunzi wa Zanzibar wanaosoma katika Vyuo vikuu hupata mikopo kutoka katika bodi ya mikopo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wengine hupata mikopo kutoka kwa bodi ya mikopo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
                                                                                MWISHO
 
 
          Serikali yakataa kuunda tume ya kuchunguza Viongozi wa dini kushambuliwa.
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema haitounda tume ya kuchunguza matukio ya viongozi wa dini waliojeruhiwa kutokana na kuwa uchunguzi huo unafanywa na jeshi la polisi na bado unaendelea.
Wajumbe hao walitaka serikali kufanya uchunguzi wa matukio mawili yaliotokea hivi karibuni katika matukio ya kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini akiwemo Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Suleiman Soraga pamoja na kujeruhiwa kwa kupigwa risasi Padre Ambros Mkenda.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa rais Mohammed Aboud Mohammed aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mwakilishi wa jimbo la Kiwani (CUF)  Hijja Hassan Hijja aliyetaka kuundwa kwa tume ya kuchunguza suala hilo pamoja na kujuwa suala la ulinzi kwa viongozi wa dini na upelelezi wake umefikiya wapi hadi sasa.
Aboud alisema katika hatua zote mbili za uchunguzi wa matukio hayo yanaendelea vizuri sana kazi ambayo inafanywa na taasisi za ulinzi ikiwemo jeshi la Polisi na hakuna sababu ya kuunda tume kwa kuwa uchunguzi huo unafanywa na jeshi la polisi.
“Taasisi za ulinzi ikiwemo Jeshi la Polisi wanaendelea na uchunguzi wa matukio ya kumwagiwa tindikali sheikh Soraga pamoja na kupigwa risasi kwa padre Mkenda, na sioni kama ipo haja ya kuingilia mamlaka nyengine katika suala hilo, nadhani tuwaachie polisi wafanye kazi hiyo na wakishakamilisha watatupa taarifa kamili ya uchunguzi wao waliofanya”alisema Aboud.
Alisema matukio hayo yameitia wasiwasi mkubwa jamii pamoja na wananchi kwa ujumla kwani yanaonesha wazi kuwepo kwa vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani.
Aboud akitoa salama za mwaka mpya kwa wajumbe na wananchi,aliwataka kuheshimu sheria za nchi na kujiepusha na kufanya vitendo vya uhalifu ikiwemo kuchukuwa sheria mikononi.
Alisema matukio mengi yalijitokeza mwaka jana ikiwemo vurugu za kidini,ambapo inaonesha wazi wananchi kushindwa kuheshimu sheria za nchi.
‘Nawaomba wananchi mwaka mpya wa 2013 kuheshimu sheria za nchi na kuacha kujiingiza na vitendo vya vurugu kwa wananchi na kiusababisha uvunjifu wa amani’alisema.
Katibu wa mufti sheikh Fadhil Soraga alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana na kuumiya vibaya sehemu ya so na kulazimika kupelekwa nje ya nchi India kwa matibabu zaidi.
Aidha padre Mkenda alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa anakaribia nyumbani kwake huko Tomondo nje ya mji wa Unguja na kulazimika kusafirishwa hadi Tanzania Bara kwa matibabu zaidi.
                                                          MWISHO
                                                     Mswada wa Maritime Authority
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwa kuzingatia usalama wananchi imeamua kufanyia marekebisho sheria zake mamlaka ya usafiri ili kulinda usalama wa baharini kwa wananchi wake.
Akiwasilisha mswada Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi kwamba “Kwa nia njema na kwa kuangalia maslahi ya wananchi wetu kiuslama na kiustawi (Safety and Comfortability) nawaomba wajumbe wa baraza lako tukufu waujadili mswada huu na kutupa mapendekezo yenye mwelekeo wa kuelekea pazuri zaidi na baadae waupitishe” alisema.
Alisema mswada huo unakusudia kufanya marekebisho na kuleta mabadiliko katika uendeshaji wa majukumu ya taasisi hiyo ya mamlaka ya usafiri wa baharini.
Aidha kuchunguza na kutilia mkazo zaidi juu ya usalama wa abiria na mabaharia katika vyombo vya usafiri na kuweka msisitizo juu ya matumizi ya vyombo vyenye uora na viwango ukilinganisha na sheria za kimataifa (IMO).
Katika mswada huo pia lengo lake ni kuendeleza ukaguzi wa kina wa kila kipindi kwa kawaida na wa ghafla pale itakapotokea haja hiyo, na kuwapata wawekezaji waliomahiri na wenye uwezo wa kukabiliana na hali inayojitokeza zinapotokea ajali au uwezo wa kujikinga.
Mamlaka ya usafiri baharini ni taasisi iliyosimama kwa sheria namba 5 ya mwaka 2006 ambapo taasisi hiyo inasimamia usajili wa meli za ndani na pia kuna usajili wa meli za kigeni ikisaidiwa na wakala huko Dubai.
Taasisi hiyo inasimamia uendeshaji wa shughuli za usafiri ikiwa pamoja na uzima na ubora wa vyombo vya baharini na hali ya usalama wa abiria na mabaharia ndani ya vyombo hivyo vinavyosafiri.
“Baada ya kutokezea ajali ya Mv Spice Islanders 2011 serikali iliunda tume na kutoa mapendekezo mbali mbali kwa bahati mbaya sana Zanzibar ilipata tena mshtuko kwa kutokezea ajali ya pili 2012 ikiwa chini ya mwaka mmoja tokea ajali ya Mv Spice Islanders” alisema Waziri huyo.
Suleiman alisema kutokana na hali hiyo ya mtafaruku ilipelekea kujichunguza upya mapungufu yaliotokea katika usimamizi wa usafiri wa bahari na aina ya vyombo vinavyotumika.
Alisema ni jambo la wazi kuwa mabadiliko yanahitajika katika kuchunga usalama wa watu na wageni wanaposafiri.
Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment