PEMBA YETU GROUP
Kikundi cha Wapemba chenye jina hilo hapo juu, kinapenda kuwajuilisheni Wapemba wote duniani kuwa kimeanzisha mradi wa kuwasaidia wananfunzi wa Kisiwa cha Pemba ambao hukabiliwa na mitihani ya Taifa kila mwaka.
Mradi huu ni wa kuwashawishi wananfunzi wanaosomea uwalimu wa chuo kikuu cha SUZA Zanzibar kwenda Pemba kuwasaidia wananfunzi wa sekondari Form 4 ambao wanakabiliwa na mitihani ya Taifa.
Ushawishi huo umefanikiwa na wamejitokeza walimu 115. Kati ya hao, walimu 105 ni wazaliwa wa Pemba, ambao tumepanga tuwasaidie usafiri. Walimu 10 ni wazaliwa wa Unguja, ambao tutahitaji kuwapatia usafiri, makaazi na chakula kwa muda watatakuwa huko. Ushawishi huu umesimamiwa na Maalim Said Yunus mwalimu katika chuo hicho, ambaye ndiyo atakuwa msimaizi na mratibu wa mradi huu.
Tayari tumeanza kukusanya kiasi fulani cha pesa ambapo jumla ya pesa zinazohitajika ni shilingi 9,050,000/=, ikiwa ni pamoja na gharama za matayarisho ya wanafunzi walimu hao.
Hivyo basi, tunawaomba Wapemba wote duniani kushiriki katika mradi huu wa kheri kwa kuchangia kiasi mtu anachoweza ili mradi huu uweze kufanikiwa. Hata hivyo, wasio Wapemba pia wanakaribishwa wakipenda kuchangia.
Kwa sasa wakusanyaji wa michango ni hawa hapa chini, na taarifa zaidi zinaweza kupatikana facebook Pemba Yetu Group. Mradi unaaza March kwa matayarisho ya mwisho na masomo April 2013.
Wapokeaji:
1. Arif Suleiman Mohammed - Daresalaam…………………..0773-556-688
2. Maalim said Yunus - Zanzibar………………………………..0776-399-494
3. Mohammed al-Nabhany – Canada……………………………(416)854-1386
4. Seif al-Khuzeiry – UK……………………...... ....…………….0794-053-4815
Email ya Pemba Yetu ni: pembayetu@gmail.com, website: www.pembayetu.wix.com/pembayetu
Wengine ni Arabuni na United States, taarifa unaweza kuzipata Pemba Yetu Group @ facebook
Kwa wale wanaoweza kutuma kwa PayPal, basi iko account ya “Pemba Yetu”
Tunatanguliza shukrani Tembelea Pemba Yetu kwa kuijua zaidi Group hii.

No comments :
Post a Comment