Written by ibnially // 24/02/2013
Jeshi la Police Zanzibar limefanikiwa kuwatia mbaroni watu watano kwa tuhuma za wizi na matukio ya kihalfu huko maeneo ya Saraevo shehia ya kisauni Unguja.
Baadhi ya mashuhada wa tukio hilo ambao hawakupenda kutajwa majina yao wamesema kua watuhumiwa hao walitoka kufanya ujambazi katika maeneo ya Tunguu jana usiku na kuja kupumzika katika chumba chao kiliopo hapo saraevo shehia ya kisauni Unguja.
Kwa mujibu wa walinzi wa Chuo kikuu cha Zanzibar University(Tunguu)wamedai kuwa watu hao walifika hapo majira ya saa kumi alfajiri na kuwafunga kamba walinzi wote wanne waliokuwepo na hatimae kuweza kuiba Computer nne aina ya Desktop za chuo hicho na wamekamatwa nazo.
Nae kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Ndugu Mussa Ali Mussa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na hadi sasa jeshi la Polisi tayari limefanikiwa kuwakamata watu watano wanaojulikana kwa majina ya,Sleiman Matius Shilimbe(32)Tomondo,Juma Ali Hamdu(32)Bububu,Khamis Said Nassor(34)Bububu,Rashid Khamis(32)Tomondo.
Aidha kamishna huyo ametowa wito kwa jamii Nchini kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha kuwa linawafichua wahalifu hapa Zanzibar.
Kwa Msaada wa Hamed Mazrouy wa Zanzibardaima na Mzalendo.net
No comments :
Post a Comment