NA JIMMY MFURU
13th March 2013
(1).jpg)
NIPASHE jana ilishuhudia wateja mbalimbali wakichukua fomu na wengine kurejesha kwa ajili ya zoezi la uhakiki katika benki za NMB,CRDB, NBC na Azania kabla ya kufungiwa akaunti zao kama hawatatekeleza zoezi hilo ifikapo keshokutwa.
Zoezi hilo ambalo lilitakiwa kukamilika mwaka jana mwanzoni, lakini kutokana na wateja wengi kushindwa kuhakikia taarifa za akaunti zao, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) liliongeza mwaka mmoja ambao utamalizika keshokutwa.
Akizungumza na NIPASHE kwa masharti ya kutotajwa jina lake gazetini, mhudumu wa benki ya CRDB tawi la Azikiwe, alisema wateja walijitokeza siku chache zilizopita.
Alisema tangu zoezi hilo liongezewe muda ni wateja wachache waliojitokeza, lakini kwa sasa wamekuwa wengi kuhofia kufungiwa akaunti zao kutokana na agizo lililotolewa na BoT.
Hata hivyo, baadhi ya wateja walionekana kutokuwa na viambatanisho vinavyotakiwa na kurudishwa na wahudumu wa benki kwa ajili ya kuwasilisha vinavyotakiwa.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment