zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, March 13, 2013

ZANZIBAR: Mvua kubwa yanyesha Unguja, Mwanafunzi apoteza maisha

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali Saidi Mwema ambaye ndiye mwenye dhamana ya usalama nchini
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali Saidi Mwema ambaye ndiye mwenye 
dhamana ya usalama nchini

Na Salma Said
MVUA kubwa imenyesha mjini hapa kuanzia usiku wa kuamkia jana na mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi amepoteza maisha…
Mwanafunzi huyo alikufa baada ya kutumbukia kwenye mtaro na mwenzake wakati walipokuwa wakilipisha gari lilolokuwa likienda kwa kasi karibu na shuleni kwao Kijitoupele nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Kaimu Kamnda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Haji Abdallah Hanna alimtaja mwanafunzi aliyekufa kuwa ni Munaifat Abdallah Mussa wa Maili Nne kati ya  Mwanakwerekwe na Fuoni.
Alisema tukio hilo lilitokea saa 1 asubuhi wakati wanafunzi hao wakitoka nyumbani kwenda shuleni.
Kamanda alisema baada ya watoto hao wawili wa shule ya msingi kutumbukia mmoja aliokolewa hapo hapo na aliyekufa alichukuliwa na maji na maiti yake ilipatikana baada ya msako uliofanywa na Zimamoto, Polisi na wananchi.
Alieleza kuwa maiti iliyokuwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja jana ilikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu na ilitarajiwa kuzikwa siku hiyo hiyo.
Kamanda aliwataka wazazi kuwachunga watoto wao katika kipindi hiki cha mvua na kuwataka madereva wa magari kuchukua hadhari wanapowaona watoto wako barabarani.

No comments :

Post a Comment