AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 15, 2013

Kamishna wa Polisi Zanzibar azungumza na vyomba vya habari

Na Masoud Ally
Kuongezeka  kwa  vitendo  vya kihalifu Zanzibar  kunawafanya  wananchi waishi kwa wasiwasi na kupelekea kurudisha nyuma  juhudi za  serikali katika  kukuza sekta  ya  utalii.
Kauli  hiyo  imetolewa leo na  kamishna wa  jeshi  lapolisi  Zanzibar ndugu  Mussa  Ali  Mussa  alipokua akizungumza  na waandishi  wahabar makao  makuu ya polisi yaliopo  ziwani  Zanzibar kufuatia matukio  mbali mbali  ya  kihalifu  yanayotokea Zanzibar.
Kamishna mussa alibainisha makosa  mbali  mbali  ya  kukamatwa  wahalifu   ikiwemo bhangi utengezaji  wa  pombe  haramu na  ujambazi  amabyo yaliyotokea mapema mwanzoni mwa mwezi wa nne  mwaka  huu.
Amebainisha kuwa  siku ya tarehe 3-4 alikamatwa Haji  Mohd Haji {35} mkaazi  wa kiboje ndukuke akiwa  kwenye  maficho  ya  kutengeneza  pombe  haramu.
Tarehe 9/4 Abdallah Shaaban  Yussuf  alikamatwa na bhangi  polo  moja  kubwa  na mapolo  madogo madogo  matatu.
Tarehe 10/4 Omar  Juma  Omar  alikamatwa  na  kete  114 zinazosadikiwa  kuwa  ni  madawa  ya  kulevya wakati  huo  huo  Omar  Said  Mohd  alishikwa  na  mabunda 29  ya  majani  makavu  yanayodaiwa kuwa ni  bhangi.
Kutokana  na mtokeo  hayo  ya  kihalifu  aidha jeshi  la polisi limefanikiwa kumtia mbaroni Faustine George {36} siku  ya  tarehe 12/4  akiwa ndani  ya  bar iliopo chuo  cha  mafunzo  mjini unguja  na kukutwa na fedha  kadhaa  za nchi mbali mbali  za kigeni pamoja  na  vifaa mbali  mbali wanavyotumia  katika masuala  ya  ujambazi.
Mtuhumiwa huyo  baada  ya  kuhojiwa saana  na  polisi ameweza kumbainisha  Mohammed  Ali Salum kwamba  ndie  anaehifadhi  mali  wanzaoziiba pamoja  ka  kuhifadhi  bunduki wanayotumia  katika masuala  yao  ya kiujambazi.
Katika  upekuzi  uliofanywa na  jeshi lapolisi wameweza  kukamata  bunduki ya  aina  ya SMG no 56-3750845 pamoja na  risasi  zake 29 na silaha  ndogo ndogo za  ujambazi  na vitu vilivoibiwa.
Mpaka sasa mtuhumiwa  Fausine  george  na  Mohammed  Ali  Salum wanashikiliwa  na jeshi  lapolisi kwa  ajili  ya mahojiano  zaidi  kuhusiana  na  mtandao wao.
Chanzo: Mzalendo.net

1 comment :

  1. Hongera jeshi la polisi, muendelee hivyo hivyo>

    ReplyDelete