Na Masoud Ally
Kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu Zanzibar kunawafanya wananchi waishi kwa wasiwasi na kupelekea kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kukuza sekta ya utalii.
Kauli hiyo imetolewa leo na kamishna wa jeshi lapolisi Zanzibar ndugu Mussa Ali Mussa alipokua akizungumza na waandishi wahabar makao makuu ya polisi yaliopo ziwani Zanzibar kufuatia matukio mbali mbali ya kihalifu yanayotokea Zanzibar.
Kamishna mussa alibainisha makosa mbali mbali ya kukamatwa wahalifu ikiwemo bhangi utengezaji wa pombe haramu na ujambazi amabyo yaliyotokea mapema mwanzoni mwa mwezi wa nne mwaka huu.
Amebainisha kuwa siku ya tarehe 3-4 alikamatwa Haji Mohd Haji {35} mkaazi wa kiboje ndukuke akiwa kwenye maficho ya kutengeneza pombe haramu.
Tarehe 9/4 Abdallah Shaaban Yussuf alikamatwa na bhangi polo moja kubwa na mapolo madogo madogo matatu.
Tarehe 10/4 Omar Juma Omar alikamatwa na kete 114 zinazosadikiwa kuwa ni madawa ya kulevya wakati huo huo Omar Said Mohd alishikwa na mabunda 29 ya majani makavu yanayodaiwa kuwa ni bhangi.
Kutokana na mtokeo hayo ya kihalifu aidha jeshi la polisi limefanikiwa kumtia mbaroni Faustine George {36} siku ya tarehe 12/4 akiwa ndani ya bar iliopo chuo cha mafunzo mjini unguja na kukutwa na fedha kadhaa za nchi mbali mbali za kigeni pamoja na vifaa mbali mbali wanavyotumia katika masuala ya ujambazi.
Mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa saana na polisi ameweza kumbainisha Mohammed Ali Salum kwamba ndie anaehifadhi mali wanzaoziiba pamoja ka kuhifadhi bunduki wanayotumia katika masuala yao ya kiujambazi.
Katika upekuzi uliofanywa na jeshi lapolisi wameweza kukamata bunduki ya aina ya SMG no 56-3750845 pamoja na risasi zake 29 na silaha ndogo ndogo za ujambazi na vitu vilivoibiwa.
Mpaka sasa mtuhumiwa Fausine george na Mohammed Ali Salum wanashikiliwa na jeshi lapolisi kwa ajili ya mahojiano zaidi kuhusiana na mtandao wao.
Chanzo: Mzalendo.net
Hongera jeshi la polisi, muendelee hivyo hivyo>
ReplyDelete