AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 18, 2013

MAFUTA YA ZANZIBAR AU YA-MUUNGANO?

Written by   //  18/04/2013 
Tumeambiwa kuwa ‘mafuta yametolewa katika orodha ya mambo ya muungano’. Tumeambiwa hivyo katika mfululizo wa vikao vingi. Cha mwisho kilikaa Zanzibar, beach resort, mara tu baada ya sherehe za mapinduzi January 12-2013, chini ya uenyekiti wa Makamo wa Rais, Dr.Bilali na huku Balozi Seif Ali Iddi.
Vilifuata vikao vya chama – CCM, pia viliridhia hilo. BLW, na Bunge limeambiwa hivyo mara elfu kidogo. Hii imekuwa nyimbo ya wanasiasa wa pande zote mbili – Tanganyika na Zanzibar.
Karibuni hivi, pinda aliliarifu Bunge kuwa ‘mafuta yametolewa katika orodha ya mambo ya Muungano’.
Msimamo wa Warioba na tume yake ya katiba ni kuwa ‘suala hilo litajadiliwa kama sehemu ya kutengeneza katika mpya’. halina haraka?
Jana, Mohammed Aboud, Waziri wa Nchi 9Zanzibar) Makamo wa PILI wa Rais aliliarifu BLW kuwa ‘bado majadiliano yanaendelea kuhusu suala hilo’ ama yawe ya Zanzibar au Muungano au…..vipi sijui. Yaani, suala hili bado halijatolewa maamuzi, ndio maana yake.
Ndugu, wana-mzalendo — TUKAMATE WAPI???
Hapa ndio panaponiuma mimi kuwa tunachukuliwa Wazanzibari just for granted, na just for ride. Na nyie wenzangu wengi mnakubali.
Hii ndio hali inayotukabili Zanzibar. Tumekosa muelekeo, tumekosa mawazo mbadala, tumekosa uongozi na viongozi.
Tumegeuzwa kama mpira wa kona. Hatuna wabunge wala wawakailishi. Ingalikuwa jana wawakilishi ni watu wenye akili timamu, na kumbukumbu, wangaliweza kumbana Mohammed Aboud atupe ukweli wa mambo: which is which???
Jamani nchi inateketea, inatutoka hiyo.
Nimeambiwa kuwa mara nyingi, ninatoa lawama, bila kushauri: nishauri nini, nimshauri nani?
Msimamo wangu au imani yangu: Tanganyika hawakubali wala hawathubutu kuyatoa mafuta katika ulingo wa muungano, na kama watayatoa, basi ni ‘kimaandishi tu’; wao ndio signatories wa mikataba yote ‘….na ushirikiana wa kimataifa….’
Tanganyika hawakubali aslan Abadan kuitoa Zanzibar au kuiwacha Zanzibar altogether. Mfanye mnavyoweza, wala msijilinganishe na ex-USSR au Yugoslavia au wapi na wapi sijui. Wale wana…………watanganyika na sisi hatuna.
Sisi tusubiri, one day, tuimbishwe Aleluyah kanisani, na tutakwenda kuimba na huku tumevaa misalaba. na Hatutokataa.
Tutabaki kucheza keram, na kupanga list wa wachezaji wa Asernal, Manchester United, Liverpool, na Real Madrid.
Tutabaki kuhadith mipira kila asubuhi tu, na nchi inazidi kututoka. Kigezo cha kuwa mstaarabu – ni kujua mpira na kuangalia mpira wa Man United, na kumhadith Sir Alex Ferguson/na upumbavu kama huo. Mtoto wa miaka saba, juzi ninamsikia anapanga list ya majina ya wachezaji wataocheza usiku wake, na ilikuwa hivyo hivyo.
Chanzo: Mzalendo

No comments :

Post a Comment