AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 18, 2013

Mbunge CCM aipinga Serikali

 Alhamisi,Aprili18  2013  
KWA UFUPI
“Mheshimiwa Naibu Spika, napingana kabisa na majibu ya Naibu Waziri kuhusu visima vya Tinde, pale kuna kisima kimoja tu na hilo la visima 24 ndiyo nalisikia leo na hata wenzake ambao wamewahi kuja kule wanalijua,”  Hamad
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu, Azza Hamad (CCM) jana aliyakataa majibu ya Serikali kuhusu visima vya maji katika Mji wa Tinde kuwa yalitolewa bila ya kufanyiwa utafiti.
Hamad alitoa kauli hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza ambapo alimweleza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri kuwa majibu yake yanapaswa kufanyiwa utafiti kwanza kabla ya kutolewa.
“Mheshimiwa Naibu Spika, napingana kabisa na majibu ya Naibu Waziri kuhusu visima vya Tinde, pale kuna kisima kimoja tu na hilo la visima 24 ndiyo nalisikia leo na hata wenzake ambao wamewahi kuja kule wanalijua,” alisisitiza Hamad.
Katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua Serikali itawasaidiaje wananchi wa Mji Mdogo wa Tinde unaokua kwa kasi ili waweze kupata maji kwa haraka wakati wanasubiri maji kutoka Ziwa Victoria.
Naibu Waziri Aggrey Mwanri alisema kuwa katika mwaka wa fedha 2012/13, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga iliidhinisha Sh39 milioni kwa ajili ya kusambaza maji katika baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo kwa kutumia kisima kirefu kilichopo katika Sekondari ya Wasichana ya Tinde.
Alisema kuwa kisima hicho kina uwezo wa kuzalisha mita sita za ujazo kwa saa na kuwa hivi kuna taratibu za kununua bomba na pampu za kusambaza maji katika eneo hilo.
“Hata hivyo, kwa sasa wananchi wa Mji wa Tinde wanapata huduma ya maji kutoka katika visima vifupi 24 vilivyojengwa kwenye vitongoji vinavyozunguka Mji wa huo,” alisema Mwanri.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri, mpango wa kuunganisha mji huo na chanzo cha maji kutoka Ziwa Victoria, uko mbioni na zabuni zake zilishafunguliwa tangu Aprili 3, mwaka huu wakati uchambuzi wa taarifa hizo ili kumpata mkandarasi unaendelea kwa sasa
.

No comments :

Post a Comment