AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, April 16, 2013

Sudan wanatakiwa kuvumiliana- Balozi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Sudan na Sudan ya Kusini waliokutana hapa Zanzibar kuzungumzia hatma ya amani ya Mataifa yao mawili
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika Picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Sudan na Sudan ya Kusini waliokutana hapa Zanzibar kuzungumzia hatma ya amani ya Mataifa yao mawili
Mataifa ya Sudan na Sudan ya Kusini yanapaswa  kuendelea kuvumiliana na kuaminiana katika masuala ya Uchumi na Utamaduni  ili kusaidia kupunguza au kuondosha kabisa  wimbi la kisiasa lililoyakumba Mataifa hayo kwa miongo kadhaa iliyopita na kusababisha Sudan ya Kusini kujitenga…
Hayo yamo katika Azimio la Zanzibar lililofikiwa mara baada ya kukamilika kwa Mkutano wa kwanza wa Viongozi Waandamizi wa Sudan na Sudan ya Kusini waliokutana  siku mbili katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Kama Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Kiongozi  wa Mkutano huo wa Viongozi waandamizi wa Mataifa ya Sudan na Sudan ya Kusini Bwana Lazaro Sumbeiywo Kutoka Nchini Kenya alisema hayo wakati akitoa muhutasari wa ripoti  ya Azimio hilo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Lazaro akiambatana na Mwakilishi wa Sudan Bwana Rabi Hassan , Profesa  Pouline Riah wa Sudan ya Kusini, pamoja na Balozi David Kapya kutoka Ofisi ya Rais Mstaafu wa Tanzania alisema mafanikio makubwa yameanza kuchomoza kufuatia Mkutano huo.
“ Tumejaribu kuweka msingi madhubuti katika mkutano wetu utakaokuwa na muelekeo wa kujenga hali ya kuaminiana na kuvumiliana katika masuala ya kisiasa kwa pande zote mbili “. Alisisitiza Bw. Lazaro.
“ Mambo matatu ya msingi tuliyoyapendekeza katika ripoti ya Azimio letu la Zanzibar  ni masuala ya Uchumi, Utamaduni na kuvumiliana katika siasa. Mipango  yote tumependekeza yakubalike kufanywa kwa pamoja “. Alifafanua Bwana Lazaro Sumbeiywo.
Kiongozi  wa Mkutano huo wa Viongozi waandamizi wa Mataifa ya Sudan na Sudan ya Kusini alimueleza Balozi Seif kwamba Mataifa hayo yanaweza kupiga hatua kubwa ya mafanikio iwapo jamii yao itaridhia kushirikiana katika masuala hayo hadi kwa wananchi wa kawaida.
Alisema Mkutano wa Pili wa Viongozi hao Waandamizi wa Sudan na Sudan ya Kusini mwezi ujao wa Mei Mjini Nairobi Nchini Kenya.
Nao Wawakilishi wa Pande hizo mbili za Sudan na Sudan na Kusini Bwana Rabi Hassan na Profesa Pouline Riah walisema Mkutano huo wa Zanzibar  umejenga Histori mpya ya kuelekea kwenye mafanikio ya kudumu ya Kisiasa kati ya pande hizo mbili.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Wananchi wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wamefarajika kuona  Mkutano huo umemalizika kwa mafanikio makubwa.
Balozi Seif alisema  Jumuiya ya Afrika Mashariki itakuwa na  fursa nzuri ya kuridhia Sudan kujiunga na Jumuiya hiyo kufuatia maamuzi ya mwanzo  ya kuzitaka Sudan zote mbili kuondoa hitilafu zao kwanza.
“ Sisi Viongozi  iwapo tutakosa  kuwa na  utulivu na uvumilivu wa kisiasa tutawezaje kuwaongoza wananchi wetu katika kuelekea kwenye maendeleo ? “. Aliuliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Balozi wa Ireland Nchini Tanzania Bibi Fionnuala Gilsennan hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo Viongozi hao wamezungumzia masuala mbali mbali ya uhusiano uliopo kati ya pande hizo mbili ambapo Balozi Fionnuala alieleza kwamba Zanzibar ina fursa nzuri ya kujifunza kwa Ireland  mfumo wa    uendeshaji wa serikali yenye muundo wa Umoja wa Kaitaifa.
Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisena Zanzibar hivi sasa imepata utulivu wa kisiasa baada ya uamuzi wake wa kufuata mfumo huo ambao bado ni mgeni miongoni mwa wananchi wake.
Alisema kumekuwa na mashirikiano mazuri ya uendeshaji Serikali miongoni mwa Mawaziri kutoka vyama vikuu viwili vilivyopata nafasi  ya kuunda Serikali baada ya uchaguzi mkuu kufuatia mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar yaliyotoa fursa  ya kuendesha Serikali yenye mfumo huo.

Chanzo: ZanzibariYetu

No comments :

Post a Comment