NA MWINYI SADALLAH
18th May 2013
.jpg)
Mpango huo umetangazwa na viongozi wa Jumuiya za CCM za Umoja wa Vijana ( UVCCM) , Umoja wa Wanawake (UWT) na ile ya Wazazi walipozungumza na wanahabari mjini Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Amour Shaka, alisema takwimu hizo zitakusanywa kutoka mikoa mbalimbali bila kujali itikadi ya chama kwa vile umaskini unawaumiza vijana bila ya kujali vyama vya kisiasa.
Naibu Katibu Mkuu huyo alisema tatizo kubwa linaloikabili Zanzibar ni kukosekana tafiti za kutambua vijana wasiokuwa na ajira na kuwawekea mazingira ya kutumia fursa za sekta binafsi kujiajiri.
Alisema serikali imeanzisha mifuko ya kuwasaidia wajasiriamali wakiwamo vijana na kuwataka kutumia nafasi hiyo ambayo imelenga kupambana na umaskini.
Naibu Katibu Mkuu wa UWT Salama Aboud Talib, alisema ziara ya Rais wa Zanzibar Dk . Ali Mohamed Shein ya mwezi uliopita katika mikoa sita ya kichama ya Zanzibar imesaidia kuwaelimisha vijana kuhusu mpango wa kujiajiri kupitia sekta binafsi.
Alisema iwapo vijana watajengewa njia bora ya kutumia fursa ya sekta binafsi, mpango wa kukuza uchumi na kupambana na umaskini utafikiwa kwa wakati visiwani Zanzibar.
Tatizo la ajira Zanzibar limekuwa na mjadala mpana na kuelezwa kuwa ndiyo chanzo cha vijana wengi kujiingiza kwenye uhalifu na utumiaji wa dawa za kulevya.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment