dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 13, 2013

Dk. Peter Dalally Kafumu

Mbunge wa Igunga, Dk. Peter Dalally Kafumu, akiwasalimia wananchi katika mkutano wa mapokezi yake uliofanyika jana jioni katika Uwanja wa Sokoine mjini Igunga mkoani Tabora. Kulia ni wa Itikadi na Uenezi na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye


Mahakama ya Rufaa yamrejesha Kafumu bungeni

10th May 2013

MbungE, Dk. Peter Dalali Kafumu (CCM) wa jimbo la Igunga.
Mahakama ya Rufaa nchini imetengua maamuzi ya mahakama kuu na kumrudishia ubunge wake Dk. Peter Dalali Kafumu (CCM) wa jimbo la Igunga baada ya kuridhika ha hoja za upande wa mrufani kuwa Jaji aliyesikiliza shauri hilo, hakuzingatia matakwa ya kisheria.

Akisoma uamunzi huo, Mwenyekiti wa jopo la majaji wa Mahakama hiyo jaji, Nathalia Kimaro, akisaidiana na jaji William Mandia na Jaji Semistrocles Kaijage, alisema  mlalamikiwa hakulipa ada ya mahakama kama sheria ya uchaguzi inavyoelekeza.

Aliongeza kuwa awali wakati shauri hilo namba 10/2011, linafunguliwa Mahakama Kuu jaji hakusikiliza pingamizi la mrufani kwamba hakukuwa na ada iliyolipwa hivyo hakupaswa kuendelea na usikilzwaji wake.

“Kutolipwa ada ama kutokuwepo kwa kumbukumbu yoyote katika jalada la mahakama inayoonyesha kitu kiwekwa kama kinga ilikuwa ni sababu tosha ya kutosikiliza shauri hilo,” walisema majaji hao katika maamuzi yao.

Katika hoja zake wakili, wa serikali Gabriel Malata za kutaka yatenguliwe maamuzi ya mahakama kuu aliwaambia  majaji wa mahakama ya rufaa kuwa jaji aliyesikiliza kesi hiyo alikosea kuanza kuisikiliza kwani mlalamikaji hakutimiza matakwa ya kisheria.

Malata alidai kuwa mlalamikaji hakulipa ada ya mahakama kiasi cha shilingi milioni moja alizotakiwa kutoa au hati ya nyumba kabla kesi hiyo haijaanza kusikilizwa kama sheria ya uchaguzi kifungu na 111 inavyoelekeza.

Wakili Malata aliongeza kuwa kwa vile mjibu Rufaa Joseph Kashindye na wenzake hakutekeleza sharti hilo usikilizwaji wa shauri hilo pamoja na mwenendo mzima yakiwamo maamuzi vyote vilikuwa ni batili.

Aliongeza kuwa malalamiko yaliyopelekwa mahakamani ni ya kutengeneza kwani hayajawahi kuwasilishwa katika kamati ya maadili ya uchaguzi kama walivyofanya juu ya suala la mbunge wa Tabora mjini, Ismali Aden Rage  ambaye alitozwa faini ya Sh. 100,000 kwa kutembea na silaha kwenye mkutano.

Hoja hizo na nyingine zilipingwa na wakili wa mjibu rufaa Profesa Abdalah Safari ambaye aliitaka mahakama ya rufaa kuzitupilia mbali na kwamba Mahakama iliyosikiliza kesi hiyo iliridhika kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria wakati wa zoezi zima la uchaguzi wa jimbo la Igunga ndipo katengua matokeo.

Kukatwa rufaa hiyo kunafuatia maamuzi ya Mahakama Kuu ya Tanzania iliyotengua matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga mkoani hapa baada ya kubainika kuwa uchaguzi huo ulitawaliwa na vitendo vya rushwa, kampeni chafu na vitisho dhidi ya wapiga kura.

Jaji Mary Shangali wa Mahakama Kuu Agosti 21, mwaka jana alitangaza kutengua matokeo hayo baada ya mahakama hiyo kuridhika na hoja saba zilizowasilishwa na upande wa mlalamikaji kati ya hoja 19 zilizowasilishwa katika mahakama hiyo.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Mlalamikaji aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)  Joseph kashindye, ambaye aliwakilishwa na wakili Maarufu nchini Profesa Abdallah Safari.

Upande wa Utetezi uliwakilishwa na  mawakili Mohamed Salum Malik na Gabriel Malata kutoka ofisi ya Mwanasheria mkuu wa serikali,Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Igunga,  na mawakili Antony Kanyama na Kamaliza Kayaga waliokuwa wakimtetea mbunge wa Igunga Dkt Peter Dalali Kafumu.

Akisoma hukumu jaji Shangali alizitaja baadhi ya kasoro zilizopelekea kutengeliwa kwa uchaguzi huo ni pamoja na  Ahadi  iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi  Dk. John Pombe Magufuli, kuhusu  ujenzi wa daraja la Mbutu ambalo alidai kwamba  kama wananchi hawataichagua CCM daraja hilo halitajengwa, wakati ambapo katika kipindi hicho kulikuwa na shida kubwa ya usafiri katika eneo hilo.

Kashndye alikubali kuridhika na maamuzi hayo huku umati wa wafuasi wa Chadema ambao ulijaa ndani ya chumba cha mahakama uliondoka kwa huzuni eneo hilo la mahakama wakikibali matokeo huku wengine wakisema tukajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao.

Kwa upande wake, Dk. Kafumu alisema hukumu iliyotewa na mahakama ya Rufaa ndio haki kamili.

Alisema kwamba amerejeshwa ubunge wake kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Igunga bila kujali Itikadi ya chama chochote cha siasa kwani waliompa kura na kumyima kura wote ni wananchi wa Igunga.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment