dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, May 13, 2013

ZANZIBAR YAFAIDIKA NA MSAADA WA EU KWA TANZANIA!

EU yaisaidia Tanzania Sh. bilioni 19

13th May 2013


Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa.
Serikali ya Tanzania imetiliana saini mkataba na Jumuiya ya  Umoja wa Ulaya ( EU) wa Sh. bilion 19 kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo cha miwa kwa wakulima wadogo Bara na vyama vya kijamii  Zanzibar kujiimarisha kiuchumi.

Mkataba huo ulisainiwa mwishoni mwa wiki na Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa na Mkuu wa ujumbe wa EU nchini, Balozi Filiberto Sebregondi.

Alisema msaada hiuo unakusudia Tanzania katika kuondoa umasikini kwa wananchi wake na kuiwezesha nchi kupiga hatua ya maendeleo kupitia sekta ya kilimo.

Waziri Mgimwa alisema msaada huo utasaidia kuwajengea wananchi uwezo  wa kutekeleza kilimo chenye tija na kupanua soko la bidhaa zitokanazo na miwa.

“Tunaushukuru Umoja wa Ulaya kwa msaada kwenye maendeleo ya nchi yetu hasa katika sekta ya kilimo cha miwa, tutaweza kuzalisha sukari kwa wingi kwa mahitaji ya taifa,” alisema.

Balozi Sebrigondi alisema EU itaendelea kuisadia Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo.


Alisema EU imeridhishwa na mikakati ya serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo na ndiyo maana imeendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kusaidia wananchi kufikia maendeleo.

“Tumesaidia sekta ya miwa ili ikue na kuchangia katika maendeleo ya Taifa, kwa kuwa Tanzania imeonyesha nia ya dhati katika kukuza uchumi wake na kuweka mazingira mazuri kwa wananchi wake ili waongeze tija katika uzalishaji,” alisema.

Alisema katika kipindi kilichopita asilimia 87 ya fedha lizizotolewa kwa Tanzania zimeshatumika katika miradi ya maendeleo, hivyo aliahidi kuwasaidia wanachi wanaojihusisha na kilimo cha miwa ili kuwajengea uwezo, kufanya tafiti na kutoa elimu ya utunzaji mazingira katika maeneo yatakayonufaika na msaada huo.

Tangu mwaka 2008 hadi 2013, EU imesaidia sekta ya kilimo Sh. bilion 25, kwa kuongeza uzalishaji wa miwa na sukari.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment