Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini
VIONGOZI wa Baraza la Manispaa la mji wa Zanzibar hawajajifunza lolote kutokana na matukio ya huko nyuma. Kwa fikra zao, bado wanaona kuwa wana haki ya kuendelea kuwaswaga wafanyabiashara wadogo kiasi cha kuwakatisha tamaa ya kuishi.
Viongozi wa baraza hili katika hali ya kawaida ungetarajia wangeshaamua kuwachukulia wafanyabiashara hawa wanaouza bidhaa mikononi kuwa ni washirika wao katika maendeleo. Hawako hivyo.
Badala yake, wanawaona wafanyabiashara wadogo hao kama kero kubwa na watu wabaya wanaostahili hasa kile kinachowafika – kukimbizwa chini ya mtutu wa bunduki sambamba na kuporwa mali zao.
Mji wa Zanzibar kama ilivyo miji mingine Afrika, umejaa wafanyabiashara vijana wanaouza bidhaa mikononi. Kwa hapa Zanzibar, wafanyabiashara hawa huitwa kwa umaarufu kama Dada njoo kwa kuwa kutwa nzima wao huwa wanapayuka kuita wateja, hususan akinadada, wanunue bidhaa.
Mitaa ya Darajani na Mlandege ina makundi makubwa ya wafanyabiashara wadogo ambao hupanga bidhaa zao njiani na kwenye maeneo ya pembezoni mwa barabara kuu na za mitaa.
Nao wangetamani kuuza bidhaa mbalimbali wakiwa ndani ya maduka yao mazuri yaliyopambwa kwa rangi zinazonukia, vioo na viyoyozi, lakini wengi wao mitaji yao ni midogo isiyotosheleza mahitaji ya kufungua maduka ya namna hiyo.
Kila mtu anakubali ukweli kwamba upangaji wa bidhaa katika staili ya kutumia njia za waenda kwa miguu au pembezoni mwa maduka rasmi, ni tatizo. Lakini si wamekuwa na sababu na kwa muda mrefu wanalalamika kuwa hawana maeneo yaliyotengenezwa kwa ajili yao? Watafanyaje sasa?
Viongozi wa manispaa wangefikiria utaratibu wa kutumia ambao utanufaisha wafanyabiashara hao na hapohapo wakanufaika wao manispaa kwa kukusanya kodi au ushuru kila siku huku mazingira ya mji yakitunzwa pia.
Manispaa imeanzisha operesheni maalum ya kuwasambaratisha wafanyabiashara hawa. Kwa kutumia askari hao wa serikali wanaobeba bunduki hadi ya aina ya Sub Machine Gun (SMG), wanawafukuza wafanyabiashara kwa mtindo wa vita, kwa lengo la kuwazuia kuuza bidhaa kwenye maeneo hayo ambayo manispaa wanasema hayatakiwi kwa biashara hiyo.
Wiki iliyopita, siku mbili hivi baada ya kusikia tangazo la manispaa kupiga marufuku biashara kwenye maeneo hayo, nilishuhudia vishindo vikubwa kati ya wafanyabiashara hawa na askari wa manispaa wakishirikiana na wale wa vikosi vya ulinzi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Katika tangazo hilo lililotolewa kwa njia ya kipaza sauti kwenye gari la wazi likiranda mtaa hadi mtaa, mtangazaji alisikika akisema kwa mfanyabiashara atakayekamatwa akifanya biashara kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, akikutwa au kupatikana na hatia, atapigwa faini ya Sh. 300,000 taslim ili kukomboa mali iliyokamatwa. Sina hakika kama adhabu hii ni katika sheria ndogo za miji.
Malori yaliyosheheni askari wenye bunduki yalipita Darajani na kuzunguka huku wakiteremshwa askari kwa nia ya kuwashughulikia wafanyabiashara wadogo hao. Hata hivyo, wafanyabiashara wenyewe wakati huo kila mmoja huwa tayari ameshatimka huku akiwa amebeba mzigo wa bidhaa zake.
Wanachofanya wafanyabiashara hao ni kunusuru bidhaa zao kushikwa kufilisiwa au kulazimika kuzilipia faini kwa ajili ya kuzikomboa. Lakini wale wanaozembea na kuchelewa kukimbia, hujikuta mikononi mwa askari, wakiwemo wa Manispaa waliobeba marungu.
Wanaokamatwa husokomezwa kwenye lori pamoja na mizigo yao na kupelekwa Makao Makuu ya Baraza la Manispaa, mtaa wa Malindi mjini Zanzibar. Hapo kuna mahakama maalum ya manispaa ambako kesi hufunguliwa, mashitaka husomwa na hukumu kutolewa dhidi ya wafanyabiashara hao.
Matukio haya yananikumbusha mambo yaliyotokea miaka kadhaa huko nyuma. Kulikuwa na mgogoro mkubwa kama huo; wafanyabiashara kwa makundi walikuwa wakiendesha shughuli zao kwenye maeneo hayo. Walionekana kero na bughdha.
Azma ya manispaa ilikuwa pia ni kulisafisha eneo hilo na kujenga bustani. Walitaka kujenga bustani mahali ambapo mamia kwa maelfu ya wananchi wanapatumia kuuza bidhaa kwa ajili ya kujikimu kimaisha. Walitaka kupageuza bustani. Masikini wee, mpaka leo mradi haujatekelezwa.
Ndipo uongozi wa manispaa ukaamua kuwaorodhesha wafanyabiashara hao kwa ajili ya kuwahamishia eneo la Kinazini ambalo wakati huo lilikuwa ni pori lililochanganyika na dampo na njia ya maji machafu yaendayo hadi baharini. Palikuwa matope matupu wakati wa mvua. Unuko ukihanikiza eneo lote.
Wafanyabiashara ambao walikuwa wengi kama walivyo sasa, walijiorodhesha ingawa wale wenye mitaji mikubwa waligoma na kufungua kesi mahakamani ambayo naambiwa mpaka sasa haijamalizika. Hawa wakubwa wao waliona hawajatendewa haki kuondoshwa mahali pa biashara na kupelekwa porini ambako hakukuwa na maandalizi yoyote kimazingira.
Katika hatua hiyo, baraza la manispaa lilipopata orodha ya wafanyabiashara waliojisajili kuwa tayari kuhamia Kinazini, likaamua kutafuta waliyemuita “mwekezaji” wa kulisafisha eneo la kulijenga miundombinu itakayowezesha kuchukua wafanyabiashara wale wengi.
Kilichokuja kufanyika ni uhuni mtupu. Kwanza, eneo hilo alipewa mtu wa nyumba kubwa katika mpango wa kifisadi ambao mwisho wake haukuwa na maana sana kwani mpaka leo eneo hilo linachefua roho kuliona lilivyo. Halina majengo ya maana isipokuwa maturubali yaliyofungwafungwa na kuzungushwa kwenye mabanda ya mbao.
Hakuna vyoo vya maana na kila siku mtu unaomba mvua isinyeshe kwa kuwa hapakaliki wala kufaa kuuzia chochote. Lakini ni hapo mtu wa nyumbani alikata mabanda na kukodisha wafanyabiashara kwa bei kubwa bila ya kujali wahitaji walio wengi ni wananchi wanaohemea pato la siku.
Matokeo yake, wafanyabiashara wengi walikimbia na baadhi yao kurudi mitaa ya Darajani kwenye wateja, huku wengine wakitafuta na kuanzisha maeneo mapya katika mitaa mingine ili kupanga bidhaa zao.
Nasema uongozi wa baraza la manispaa unatakiwa kubadilika. Wafanyabiashara wadogo wanahangaikia maisha baada ya kukosa ajira rasmi za kufanya. Wanachotaka ni kusaidiwa kufanya biashara zao kwa mpangilio mzuri hivyo kupata mapato ya maana huku wakilipa kodi.
Hivi manispaa wangejengea jumba kubwa la kisasa na kukata milango kwa ajili ya kuwapangisha wafanyabiashara hao wangekosa nini? Hawaoni kwamba kwa kufukuzana na kukimbizana na wafanyabiashara kila siku ni kupoteza muda na raslimali haba walizonazo kwa ajili ya miradi ya maendeleo?
Nazungumzia jumba la kimachinga kama yaliyojengwa kwengineko duniani. Jumba ambalo kila huduma itapatikana humo – choo, bafu, sehemu za kula na kunywa, benki, maduka ya kubadilisha fedha na taasisi za kutoa mikopo, mama lishe, maduka ya kisasa ya bidhaa mchanganyiko, masoko madogo, saluni, sehemu za kuegesha magari.
Eneo kama hilo linavuta watu kufika. Watu wakifika watapata nafasi ya kuona bidhaa ziuzwazo na wafanyabiashara wadogo hawa. Watanunua na kurudi nyumbani na furaha. Wafanyabiashara nao watakuza mitaji yao kutokana na faida waipatayo kila mwezi. Biashara zitakua na mapato yataongezeka kwa manispaa.
Huu ni mpango wa kiuchumi. Mpango wa kuongeza mapato kwa manispaa na kuwasaidia wafanyabiashara wazawa kuendesha maisha yao. Kwa mpango huo, hakutakuwa tena na fukuza kimbiza kama inavyotokea leo. Utakuwa ni mpango wa ushirika wa wafanyabiashara na manispaa. Watakuwa rafiki wa maendeleo badala ya adui ndani ya vikwazo vya kuendelea.
Kitu kinachosikitisha ni kushuhudia askari wakipora mali za wafanyabiashara ambao wengi wamekopa mikopo ya viwango vidogo na kuhitajika kurudisha fedha kila wiki. Mara kadhaa askari wanakutwa njiani wakiwa wamebeba mikoba waliyojaza bidhaa ambazo zimeibwa kutoka kwa wafanyabiashara wanaoganga njaa.
Huu ni uhalifu na unyang’anyi wa mali za watu masikini. Kwa sababu hiyo, manispaa itaendelea kuonekana kama taasisi ya kunyang’anya wafanyabiashara wanaojiajiri kwa kukopa ili kupata fedha za kujikimu kimaisha.
Huu si mtindo mzuri hata kidogo. Haupaswi kuendelea. Tena, ukiendelea hivyo, najua ipo siku isiyo jina wala tarehe, wafanyabiashara wanyonge watakataa kwa kusema “basi imetosha.” Watajitetea japo wanajua watalazimika kutunishiana misuli na majabari wenye bunduki. Nani anajua kitakachotokea?

Kwa kujua fika kuwa nazungumzia mradi mkubwa wa maendeleo, na kwa kuwa imani yangu ni ndogo kwamba Baraza la Manispaa wanaweza kuutekeleza kwa ufanisi, ni wakati muafaka kwa wizara inayosimamia mabaraza ya miji kuzingatia mawazo haya na kuchukua hatua ili kubadilisha sura ya eneo na kukoma mtindo wa kukimbizana kusikokwisha ambako hakuna anayenufaika kati ya pande hizi mbili.
Chanzo: ZanzibariYetu
No comments :
Post a Comment