dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, August 26, 2013

Kesi ya kufutwa Muungano yatajwa Z’bar

Written by   //  25/08/2013 

vijana_muungano
Kesi hiyo ilitajwa mbele ya Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi kwa vile anayepaswa kuisikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu hakuwepo mahakamani.
Zanzibar. Kesi ya aina yake ya kikatiba inayotaka Muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika ufutwe imetajwa Mahakama Kuu Zanzibar huku wadai wakieleza kuwa kesi yao inacheleweshwa.
Kesi hiyo ilitajwa mbele ya Mrajis wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi kwa vile anayepaswa kuisikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu hakuwepo mahakamani.
Wakili wa watu 1,950 wa Unguja na Pemba waliofungua kesi hiyo, Philip Ojode wa Mombasa Kenya alidai kuwa miezi minne sasa imepita tangu kesi hiyo kufunguliwa mahakamani lakini haijasikilizwa.
Alimtaka Mrajis wa Mahakama Kuu Zanzibar kuto amri kwa wadaiwa katika kesi hiyo ambao miongoni mwao ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kwa kuwapa siku saba kujibu maelezo ya kesi hiyo.
Wakili wa Serikali, Mark Mulwambo anayesaidiwa na Fatma Salehe alidai kuwa Mrajis wa Mahakama Kuu hana mamlaka ya kutoa amri yoyote katika kesi hiyo.
Mrajis Kazi alisema kuwa ni kweli yeye hana mamlaka ya kutoa amri yoyote kuhusiana na kesi kwa vile mamlaka hayo yako kwa majaji wa Mahakama Kuu na hivyo hawezi kutoa uamuzi.
Mrajisi wa Mahakama Kuu aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 13,2013 kwa kusikilizwa na Jaji Mkuu ambaye ilielezwa jana kuwa alipata safari ya ghafla ya kwenda Dar es Salam.
Mara ya mwisho ilipotajwa kesi hiyo Julai 25 mwaka huu mbele ya Mrajis wa Mahakama Kuu, Jaji Mkuu alikuwa safarini Kagera kushiriki sherehe za kitaifa za siku ya mashujaa.
Chanzo: Mzalendo

1 comment :

  1. Ni kweli kwamba wakili wa Wanaharakati ameamua kuondoka kusimamia hii kesi?

    ReplyDelete