Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, August 6, 2013

TENDWA ANG’OKA

Tendwa

JAJI wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Francis Mutungi,  ameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Taarifa ya uteuzi huo iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,  Ikulu na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, ilisema kuwa  uteuzi huo ulianza Agosti 2, mwaka huu.
Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama  vya Siasa, John Tendwa, ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa  sheria.
Uteuzi huo unamfanya Jaji Mutungi kuwa msajili wa tatu tangu kurejeshwa tena  mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1992.
Aliyekuwa wa kwanza kukalia ofisi hiyo ya msajili ni Jaji mstaafu, George  Liundi, kisha akafuatiwa na Tendwa, ambaye amerithiwa na Jaji Mutungi.
Jaji huyo aliwahi kuwa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na  Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania.
Wapinzani wasifu
Kufuatia uteuzi huo mpya, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  kimesema kuwa Tendwa alipaswa kuwa ameondoka ofisini tangu mwaka 2008  alipofikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Tarifa ya Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya chama hicho imesema kuwa Tendwa  alitumia muda huo wa miezi kadhaa alipoongezewa mkataba kuropoka na kuharibu  demokrasia kwa manufaa ya Rais Kikwete na CCM.
CHADEMA iliongeza kuwa kutokana na mwenendo wake mbovu, chama hicho  kilitangaza kutokumpatia ushirikiano wowote kwa vile alikuwa adui wa demokrasia  nchini.
“Kwa muda wote huo, CHADEMA ilikuwa ikitoa ushirikiano kwa Ofisi ya Msajili  wa Vyama vya Siasa. Badala ya kuifuta CHADEMA na kufanikisha dhamira ovu ya  kuharibu amani ya nchi, ameondoka yeye,” ilisema taarifa ya CHADEMA.
CHADEMA ilisema kuwa wanamkaribisha Jaji Mutungi kwenye kazi na majukumu yake  mapya. Kwamba, wapenda demokrasia na maendeleo nchini wanamtarajia atatimiza  wajibu wake kwa kuzingatia haki, sheria na utawala bora, asije akapita njia ya  Tendwa.
“Kupitia mchakato wa Katiba mpya unaojadiliwa sasa hivi, CHADEMA  tunapendekeza Ofisi ya Msajili ipewe uhuru zaidi na uteuzi wake usiwe suala la  rais kuamka tu na kuamua kuteua bila wahusika kuomba, kuchujwa na kuthibitishwa  na mamlaka nyingine tofauti na iliyoteua,” walisema.
Jaji Mutungi, anapaswa kuonesha kwa maneno na vitendo kwamba hatakuwa kama  Tendwa, kwa kuanza kushughulikia matendo ya kiharamia yaliyofanywa na Green  Guards wa CCM kwenye chaguzi za madiwani zilizomalizika hivi karibuni.
Naibu Mkurugenzi wa Uenezi na Haki za Binadamu wa Chama cha Wananchi (CUF),  Abdul Kambaya, alisema ni jambo zuri ingawa aliyemteua vilevile ni Mwenyekiti wa  CCM, hatua ambayo inaleta hofu kidogo.
“Tunadhani ni mtu mweledi, sisi hatupigi ramli kuhusu utendaji wake, mpaka  tutakapomwona akianza kazi. Wakati wa Tendwa tumefanya kazi katika mazingira  magumu, hasa sisi wapinzani, tunaomba huyu asifuate hayo. Tendwa aliiogopa sana  CCM,” alisema.
Naye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Sam Ruhuza, alisema wanamtakia kila jema  Tendwa na kumkaribisha kwa furaha Jaji Mutungi, japokuwa wateule wote huwa  wanafanya kazi ya kumpendeza aliyewateua..
Chanzo: TANZANIA Daima

No comments :

Post a Comment