Written by Ashakh (Kiongozi) // 06/08/2013
Imeandikwa na Baba wa Taifa
Hivi karibuni kumezuka mtindo wa wizara ya fedha au wizara yenye mamlaka ya wafanyakazi wa serikali kufanya uhakiki wa wafanyakazi wao. Kinachoangaliwa ni:
Kiwango cha elimu kama ni sahihi au kama hawakughushi vyeti; umri wao mnasaba na vyeti vyao vya kuzaliwa (wengine wameghushi umri ili kuongeza muda wa kufanya kazi serikalini zaidi na zaidi); mishahara yao – wengine mishahara wanayopokea hailingani na elimu zao: diploma atalipwa mshara wa digrii, na wa digrii analipwa wa cheti inategemea umeegemea wapi kisiasa au ukaribu wako na watendaji wakuu wa wizara.
Mfano mzuri tu ni wizara ya elimu. hii imeoza kwa mishahara hewa na wafanyakazi hewa. Kimantiki, haiwezekani kuwa na mfanyakazi hewa au mishahara hewa bila watendaji wa wizara kuhusika. Haiwezekani aslan abadan.
Zoezi hili la kuhakiki wafanyakazi wa serikali limefurutu ada has mwezi huu wa Ramadhan. Walimu wanakwenda kupiga magoti katika vituo mbali mbali kwa madai kuwa wanasubiri kuhakikiwa au kusubiri mishahara yao.
Juzi tu, walimu wa Kiembe Samaki walikaa mpaka saa tatu usiku eti wanasubiri watoaji wa mishahara na kuhakikiwa. Baadhi yao tumewauliza ‘mmefutari wapi’ je, hao waliokuiteni wao ni waislamu (wanafunga au hawafungi). Hizi ni adhabu ambazo si za lazima kwa watendaji wa serikali, ni ubovu wa watendaji wetu wa serikali, wanaonekana kuwa sio mahiri wa kumudu kazi zao walizopangiwa.
Hivi kila siku wafanyakazi hawa wanahakikiwa lakini uoza unabaki pale pale. Isitoshe, hawa watendaji wa wizara ya elimu hawana record za nyuma, maana umemhakiki mwalimu, mwezi wa februari, halafu, mwezi wa Juni, baadaye julai, na unauliza maswali hayo hayo kila siku, ukiuliza wanakwambia ‘computer zetu imeharibika’ au hawana kabisa kumbukumbu.
Hapa ipo namna. Ama watendaji wa wizara husika wana mpango na wao kufanya ‘magube magube’ au ni sehemu ya mtandao wa huo wizi unaofanyika na ghilba za wafanya kazi hewa.
Hivi kwa nini hatujasikia hata mwalimu mmoja au mtendaji wa wizara husika amefukuzwa kazi au ameadabishwa kw akosa kama hili, ilhali wanajulikana?
Tukumbuke kuwa athari ya zoezi hili lisilokwisha ni mambo mengi:_
Baba wa Taifa
Wengi wa walimu hawa wanachukua mishahara yao benki, na sasa benki hiyo PBZ imekosa biashara.
Chanzo: Mzalendo
No comments :
Post a Comment