Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 9, 2013

NBC yazindua promosheni `Weka Upewe' ya mil. 300/-

NA MWANDISHI WETU

9th October 2013


Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa wa NBC, Andrew Massawe (kulia), akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa promosheni ya �Weka Upewe� ya NBC jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Mfugale na kushoto ni Meneja katika kitengo hicho, Dorothea Mabonye.
Benki ya NBC, imezindua promosheni ya miezi mitatu ya kuweka akiba iitwayo `Weka Upewe' itakayogharimu zaidi ya Sh. milioni 300 yenye lengo la kuhamasisha wateja wake kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba.

Promosheni hiyo ni moja ya matukio ya kuadhimisha Mwezi wa Huduma kwa Wajeja wa NBC.

 Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Mwinda Kiula Mfugale, alisema benki hiyo ipo katika kipindi cha kufurahi na wateja wake kwa kuonyesha umuhimu wao kwa kuwaunga mkono katika kipindi chote cha huduma zao nchi nzima.

“Kampeni hii si tu ina nia ya kufurahi na wateja wake kwa kuwaunga mkono, lakini pia kuwafanya wateja wawe na utamaduni wa kutunza na kujiwekea akiba kwa manufaa ya baadaye," alisema.
Alisema wanatarajia kwamba wateja wao watajitokeza kwa wingi kuweka akiba katika akaunti ya malengo na amana maalum ambapo watajishindia zawadi mbalimbali ikiwamo pikipiki, jenereta na gari aina ya Suzuki Swift.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za kuwekeza na wateja wakubwa, Andrew Massawe, alisema wateja wa benki hiyo kupitia promosheni hiyo, watajifunza kuweka akiba kwa maisha ya baadaye.

“Kutokana na mazingira ya sasa ya kiuchumi, ni muhimu kwa wateja wetu kujifunza namna ya kuweka akiba na matumizi bora ya fedha ikiwamo kuwa na bajeti katika maisha yao ya kila siku,” alisema.

Alifafanua kuwa katika kipindi hiki cha   miezi mitatu ya promosheni, watapatikana washindi sita na ili mteja awe mshiriki atatakiwa kufungua akaunti ya malengo au ya amana ya malengo ambayo ni ya mwaka mmoja.

Aidha, alisema promosheni hiyo pia inaweza kuwanufaisha wateja wapya.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment