Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 10, 2013

Rais Kikwete amaliza mvutano Hospitali ya Tumbi

NA WAANDISHI WETU

10th October 2013


Rais Jakaya Kikwete
Ziara ya Rais Jakaya Kikwete  wilayani Kibaha, mkoani Pwani imesaidia kumaliza mvutano baina ya Shirika la Elimu Kibaha na uongozi wa mkoa na wilaya hiyo kuhusiana na Hospitali ya Tumbi.

Akizungumzia tatizo hilo, Rais Kikwete alisema hali hiyo inasababishwa na utata baina ya viongozi ambao wanadai kuwa Hospitali ya Tumbi ni ya Shirika la Elimu Kibaha (KEC) na si ya serikali. Akizungumza mjini Kibaha juzi akiwa katika siku ya tano ya ziara yake mkoani Pwani, Rais Kikwete aliwashukia watendaji wa mkoa, wilaya na KEC kwamba ndiyo chanzo cha kuyumbisha juhudi za serikali za kuboresha huduma za afya.

Hatua hiyo ya Rais Kikwete ilitokana na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini, Sylvestry Koka kueleza kuwa wananchi wamekuwa wakinyimwa huduma ya matibabu katika Hospitali ya Tumbi kwa madai kwamba imeshakuwa hospitali ya rufaa.

Alisema hali hiyo imekuwa ikisababisha msongamano mkubwa wa wagonjwa katika vituo vingine vya afya huku wagonjwa hususani wajawazito wakilala watatu kitanda kimoja na wengine chini.

Rais Kikwete aliwataka viongozi wote kuelekeza jitihada zao kujenga hospitali ya wilaya na kwamba Hospitali ya Tumbi ni ya mkoa kwani shirika ni mali ya serikali.

“Niliwahi kusikia mnatembeza bakuli, mkamtumia Mzee  Ally Hassan Mwinyi, mliniomba mchango nikakataa kutoa na leo ndiyo nawaeleza sababu, kwamba serikali inautaratibu wake na haiwezi kujenga hospitali ya mkoa kwa kutembeza bakuli” alisena na kuongeza:

“Hospitali za mkoa zinajengwa kwa fedha za serikali kuu, nyie viongozi mlijichanganya wenyewe kutokana na fikra kwamba Tumbi ni hospitali ya Shirika la Elimu Kibaha, ndio maana mmeshindwa kupata fedha za kujenga hospitali ya mkoa.’’

Mvutano huo ulikuwa ukisababisha wagonjwa kurundikana katika Kituo cha Afya Mkoani, huku Hospitali ya Tumbi ikibaki bila wagonjwa ikihudumia watu  wanaopata ajali katika barabara kuu za Morogoro na Chalinze/Segera.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment