NA WAANDISHI WETU
19th October 2013
B-pepe
Chapa

Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) na Kampuni ya uzalishaji umeme ya Zwart Techniek ya Uholanzi, zimetiliana saini ya kuanzisha mradi wa umeme katika mikoa ya Kagera na Rukwa utakaogharimu Sh.bilioni 66.
Mradi huo utazalisha umeme wa megawati 7.5 katika wilaya za Ngara, Biharamulo (Kagera) na Mpanda (Rukwa), ujenzi unaotarajiwa kuanza mwezi Novemba, mwaka huu.
Akizungumza wakati wa uwekaji saini jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alisema kuanzishwa kwa kituo hicho ni moja ya mikakati ya serikali iliyoahidi kupambana na tatizo la umeme nchini hususani mikoa ambayo haina umeme wa uhakika na vijijini.
Maswi alisema kwa sasa serikali ina mpango wa kupeleka umeme katika mikoa ya Ruvuma na Njombe ambayo haina gridi ya taifa hususani Songea na Makambako, na mkataba unatarajiwa kufanyika mwezi huu.Mradi huo utazalisha umeme wa megawati 7.5 katika wilaya za Ngara, Biharamulo (Kagera) na Mpanda (Rukwa), ujenzi unaotarajiwa kuanza mwezi Novemba, mwaka huu.
Akizungumza wakati wa uwekaji saini jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alisema kuanzishwa kwa kituo hicho ni moja ya mikakati ya serikali iliyoahidi kupambana na tatizo la umeme nchini hususani mikoa ambayo haina umeme wa uhakika na vijijini.
“Shirika letu la umeme limejipanga kusambaza umeme kwenye mikoa yote na hivi sasa mikoa ya Lindi na Mtwara tayari imefikiwa hivyo hakuna mkoa utakaoachwa kwenye mpango huu na matokeo makubwa sasa,” alisema Maswi.
Aliongeza kuwa fedha za mradi huo zitachangiwa na serikali zote mbili za Tanzania ambayo imetoa asilimia 50 na Uholanzi asilimia 50.
Kwa upande wake, balozi wa Uholanzi nchini, Jaap Fredriks, alisema urafiki wa Uholanzi na Tanzania ulianza muda mrefu na utaendelea kudumu, na kueleza kuwa mradi huo wa ufuaji umeme utaleta manufaa kwa nchi zote mbili sio Tanzania peke yake.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment