Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 6, 2013

URANIUM: Wataalamu waitaka Tanzania kuachana na mpango wa Urani

NA MWANDISHI WETU

6th October 2013


Wataalam wa masuala ya madini na nyuklia, wameitaka Serikali ya Tanzania kusitisha mara moja mpango wa kuchimba madini ya Urani kwa kuwa hayana faida kubwa kiuchumi na hasara zake ni nyingi kwa afya na mazingira.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam, katika hitimisho la Kongamano la Kimataifa kuhusu uchimbaji wa madini ya Urani na athari zake kiafya na mazingira.
Mwanafizikia David Fig , alisema mataifa mengi duniani yanapinga uchimbaji wa madini ya Urani ambapo tayari Ujerumani na Switzerland zimeshaachana na mpango huo, Italia inaelekea kuacha na Japani ilishafunga vituo vyake 54 kutokana na madhara yaliyotokea Fukushima.

Alisema athari za madini hayo ni kubwa na tofauti na jinsi watu tunavyosikia ama kuelewa kwa akili zetu za kawaida, maji yenye sumu yamekuwa yakitiririka na kuharibu viumbe vya majini na mazao, hasa kipindi cha mvua, kukausha mimea, kuharibu na kupoteza rutuba kisha kupelekea magonjwa mbalimbali ya ajabu na vifo vya watu wasio na hatia.
Mkuu wa Shirika la Green Niger, Silli Ramatou, kutoka nchini Niger alisema nchi za Afrika ni masikini na hazijafikia kiwango cha kuweza kuzuia ama kufidia mazara mbalimbali yatakayosababishwa na athari za madini ya Urani.
“Tumeshuhudia watu wanaoishi kwenye mazingira ya uchimbaji wa madini kama vile dhahabu, ambayo athari zake ni ndogo sana, wakitaabika na kuonekana kama si kitu, japo kuwa ardhi yao imekuwa ikiwanufaisha baadhi ya watu, ndiyo tutaweza kuwafidia watu watakao athirika na madhara ya madini ya Urani,” alisema.
Kwa upande wa wananchi, wameitaka serikali kuhakikisha inatengeneza kwanza sera na sheria maalum za uchimbaji wa madini hayo, kabla ya kuanza mpango wa uchimbaji wa madini hatari ya Urani.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment