Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 16, 2013

Viongozi Afrika isaidieni ICC, msiikimbie

NA MHARIRI

16th October 2013


Katuni
Ni dhahiri viongozi wa bara la Afrika wamekasirishwa kama siyo kuchoshwa na kile wanachodai uonevu wa Mahakama Makosa ya Kijinai ya Umoja wa Mataifa (ICC). 

Katika kuonyesha kuchoshwa kwao, kwenye mkutano wa Umoja wa Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia wiki iliyopita waliazimia kuwa kuanzia sasa hakuna kiongozi wa bara hilo aliyeko madarakani atakayefika kwenye mahakama hiyo kusikiliza kesi dhidi yake.

Viongozi hao waliungana na kilio cha Kenya kwamba viongozi wake wakuu, Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais, William Ruto, kutokuhudhuria kesi dhidi yao zinazowakabili huko The Hague, makao makuu ya mahakama hiyo, hadi hapo watakapomaliza muda wao wa utawala. 

Uhuru na Kenyatta pamoja na mtangazaji wa Redio Kass FM, Joshua Sang, wanakabiliwa na makosa ya kuchochea mauaji baada ya uchaguzi mkuu wa urais nchini Kenya, mwaka 2007 na mwanzoni mwa mwaka 2008.
Viongozi hao pia wameitaka Kenya na kwa kweli wanaiunga mkono wawasilishe maombi yao rasmi kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kusitishwa kwa kesi inayowakabili hadi watakapomaliza muda wao wa utawala.

Kilio kikuu cha viongozi wa Afrika ni kwamba ICC imekuwa inawabagua viongozi wa Kiafrika tu kwa kuwaundia mashitaka na kuwataka kufika mahakamani. Mbali na Uhuru na Ruto, pia mahakama hiyo imekwisha kutoa hati ya kukamatwa kwa Rais wa Sudan, Omar al Bashir, kutokana na makosa ya kivita katika jimbo la Darfur, ambako maelfu ya watu wameuawa na wanamgambo wa Janjawid kwa miaka zaidi ya 10 sasa.

Pia ICC ilikwisha kusikiliza kesi ya aliyekuwa Rais wa Liberia, Charles Taylor juu ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone ambako malaki ya raia wa nchi hiyo waliuawa na wengine kukatwa viungo katika vita ambayo Taylor anadaiwa kuwa alihusika kusaidia kuendeleza ili anufaike na madini ya almasi yaliyokuwa yanapatikana kwa wingi nchini humo.

Taylor alihukumiwa kifungo cha miaka 50 jela na alikata rufaa, lakini alishindwa tena na sasa anatumikia kifungo nchini Uingereza ingawa mwenyewe ameomba ahamishwe Rwanda kutumikia kifungo hicho ili iwe rahisi kwa ndugu zake kumtembelea.

Ingawa viongozi wa Afrika wanapaza sauti na kuonyesha umoja wao dhidi ya ICC, pia wakieleza kuwa wanalengwa wao tu, wapo baadhi ya viongozi wengine nje ya bara hilo ambao walifikishwa kwenye mahakama hiyo.
Miongoni mwao ni aliyekuwa Rais wa Serbia kati ya mwaka 1989-1997, Slobodan Miloševic. Alikuwa pia Rais wa Shirikisho la Yugoslavia kuanzia mwaka 1997 hadi 2000.

Ingawa Miloševic alifikishwa ICC kwa makosa ya uhalifu wa kivita, kesi yake haikufika mwisho kwa sababu ya kifo chake akiwa mahabusu. Hata hivyo, majenerali wake akiwamo Ratko Mladic, walishitakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita. Naye Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, anakabiliwa na mashitaka ya makosa ya ukatili wa kivita na mauaji.

Ingawa viongozi walioko madarakani wa Afrika wanaitumia AU kuwasilisha kilio chao dhidi ya ICC, na pia wakionyesha uonevu mkubwa dhidi yao, wapo viongozi wa bara hilo ambao wamekaa madarakani na kustaafu uongozi ama kwa ridhaa yao au kwa mujibu wa katiba za nchi yao na wangali wanaishi maisha ya amani na utulivu katika nchi zao tena wakiheshimiwa na wote.

Miongoni mwa viongozi hawa wapo ambao walistaafu baada ya ICC iliyozaliwa kutokana na mkataba wa Rome ulioanza kutekelezwa Julai 2002.

Hawa ni pamoja na Rais wa awamu ya Tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, Rais mstaafu wa Msumbiji, Joachim Chissano, Rais Mstaafu wa Nigeria, Olusegun Obasanjo, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, Rais Mstaafu wa Namibia, Sam Nujoma, Rais Mstaafu wa Namibia, Festus Mugae wa Botswana, Jerry Rowlings na John Kufour wote wa  Ghana na Balili Muluzi wa Malawi, kutaja kwa uchache tu.

Viongozi hao wastaafu wengine wakiwa wamejishindia tuzo ya utawala bora ya Taasisi ya Mo Ibrahim, kama Chissano na Mogae, siyo tu wameendelea kuishi katika nchi walizoongoza bila kubughudhiwa na raia wao au watawa waliowafuata hata kama walitoka chama cha upinzani kama Ghana, lakini pia wametumia na Umoja wa Mataifa kufanya shughuli mbalimbali za upatanishi katika migogoro ya Afrika mingi ikiwa ni ya kugombea madaraka.

Sisi tunasema na kama ambavyo jana tuliripoti katika gazeti hili tukiwanukuu wataalam mbalimbali wa masuala ya mahusiano ya kimataifa kwamba viongozi wa bara hilo hawana sababu ya kuishuku ICC  kama kweli wanaendesha/wanatawala nchi zao kwa misingi ya utawala bora.

Ndiyo maana wastaafu wengine ambao wamekuwako baada ya kuanza kwa ICC hawana hofu, wanaendelea kuenziwa na kuheshimiwa.

Hatua na kampeni zinazopigwa na viongozi hawa zinaweza kuelezwa kuwa ni jitihada za kujificha na kuhalalisha udhaifu wa tawala zao, hasa kwenye suala zima la haki za binadamu kudumisha demokrasia na utawala bora.
Ni jambo la bahati mbaya kwamba wapo viongozi walioapa kwenye majukwaa ya kuomba kura kwamba hawaogopi kwenda kujitetea ICC kwa sababu wanajua kuwa hawana hatia, lakini leo wanaongoza kampeni za wazi na chini chini za kutaka kesi dhidi yao ama zifutwe au zisubiri wamalize muda wao wa utawala.

Wakati kauli kama hizi zikitolewa na baadhi ya viongozi wa Kiafrika wakiwaunga mkono, wanasahau kwamba wapo raia walioathirika na vurugu zao ambazo zilisababisha kuuawa kwa ndugu zao, kujeruhiwa na hata mali zao kuteketezwa kwa maslahi ya kisiasa.

Tunaamini kila mtuhumiwa ni msafi mbele ya sheria hadi athibitike kinyume chake, tunawaomba viongozi wa Afrika wawafikirie raia wao zaidi kuliko kujitazama wao tu na madaraka yao.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment