NA JOHN NGUNGE
4th November 2013
.jpg)
Katika taarifa yake fupi kwa vyombo vya habari iliyotolewa mwishoni mwa wiki kuhusu 'Hali ya mambo katika Jumuiya' Dk. Sezibera, alisema malalamiko hayo yatazungumzwa katika kikao cha 28 cha Baraza la Mawaziri kinachotarajiwa kufanyika Novemba 28, mwaka huu. Alisema kikoa hicho kitatoa mapendekezo kwa mkutano mkuu.
Alisema katika moyo wa kujenga na kuimarisha mtangamano wa jumuiya, mawaziri hao wamepeana taarifa kuhusu yaliyojiri kwenye mikutano hiyo na changamoto zilizojitokeza.
Alisema hivi karibuni kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusu mikutano kadhaa ya viongozi wa nchi za Rwanda, Uganda na Kenya iliyokuwa ikifanywa bila kuwashirikisa marais wa Tanzania na Burundi.
Alisema nchi wanachama zimekubaliana kutekeleza mikataba ya soko la pamoja na umoja wa forodha na kuondoa vikwazo katika biashara pamoja na uhuru wa watu kwenda nchi nyingine.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment