NA MWANDISHI WETU
4th November 2013

Naibu wa Waziri, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alisema hayo wakati akifunga kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TTCL jijini Dar es Salaam.
Alisema ni nia ya serikali kuona inamiliki TTCL kwa asilimia 100.
“Kwa sasa shirika hili lina miundombinu yote na uwezo wa kufanya kazi vyema,” alisema. Kwa sasa kampuni ya Airtel inamiliki asilimia 65 wakati TTCL inamiliki asilimia 35.
Aliongeza kusema kuwa ni dhamira ya wizara na serikali kuona TTCL inashika hatamu katika kuongoza sekta ya mawasiliano hapa nchini ili kufikisha huduma hiyo sehemu zote za nchi.
Aliitaka kampuni hiyo kuingia katika teknolojia ya masafa ya GSM ambayo yanawezesha wateja kutumia simu moja kwa laini zaidi ya moja tofauti na teknolojia inayotumika sasa ya CDMA ambayo inatumia laini moja tu.
Alisisitiza kwamba serikali itaiwezesha kampuni kupata mkopo kwa ajili ya kufikia malengo yake hayo ili kuzidi kutoa huduma bora kwa Watanzania.
Pia alipongeza kampuni hiyo kwa kutoa huduma bora ya mkongo na aliagiza uongozi kuzidi kuutunza na kutafuta masoko zaidi ili watu wazidi kupata huduma za mawasiliano yakiwamo ya intaneti kwa ufanisi na urahisi.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment