Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 21, 2013

CHADEMA WAKITAKA WASITAKE - ZITTO KABWE FOR THE PRESIDENCY IN 2015!!!

ZITTO KABWE - THE 2015 PRESIDENTIAL CANDIDATE OF CHADEMA.
SISI TUNASEMA: "DR SLAA USIWE KAMA MAALIM SEIF, TAFADHALI ACHIA NAFASI VIJANA
TUPATE KUREJESHA MABILIONI YA PESA YALIOPO SWITZERLAND!!!"

 

Mhe Zitto Kabwe leo ameandika historia kwenye aridhi ya Kigoma baada ya kupata Mapokezi ambayo wenyeji/wazawa wanadai labda Nyerere ndio aliyapata mapokezi haya.
Mh.Zitto amerejea leo Kigoma kuzungumza na wananchi wake,wananchi wote wa Kigoma namna mwenendo wa siasa ndani ya CHADEMA unavyorudisha utafutaji wa Demokrasia makini ndani ya Nchi hii,Pia namna wanachadema wenzake wanavyopigilia misumali kwenye mwili wake ilikukwamisha jitihada zake za kupambana na mafisadi,Kupambana na ujenzi wa Taifa letu.

Mh.Zitto Kabwe amaetua Kigoma mnamo saa 3 na Nusu Asubuhi ambapo alikutana na Maelfu ya wananchi wakiwa Nje ya uwanja wa Ndege tayari kwa kumpokea.

Maandamano ya Amani yaliyojumuisha maelfu ya Wanakigoma,kukiwa na pikipiki zaidi ya 240 na magari ya Watu Binafsi wenye mapenzi ya dhati kwa zitto zaidi ya 80 yalianza safari ya kutoa Airport kupitia Ofisi za Mkoa za CHADEMA na hatimaye safari ya kuelekea Kigoma Kaskazini kijiji cha Mwandinga alipozaliwa Zitto Kabwe kwaajili ya Mkutano wa Hadhara kuzungumza na wananchi wake.

Maandamano hayo ya Amani/msafara uliochukua zaidi ya masaa 3 kwa kutembea zaidi ya Kilomita 15 kwa mwendo wa polepole hatimaye ukafika Mwandinga.

Kwwenye Mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na maelfu ya Wananchi wakitokea pande zote za Kigoma,Zitto alijikita kwenye mambo Makuu Matatu,Kwanza kueleza kwanini ameamua kurejea Nyumbani (Kuzungumza na waliompatia Ubunge),Pili kuzungumzia hali ya Kisasa anayopitia kwa sasa ambapo amekili yeye bado ni mwanachadema Mtiifu sana,Na anaamini Rufaa yake kwa Kamati kuu chombo cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya chama kitamtendea haki,kwa sababu tuhuma zote dhidi yake sizakweli,Pia zimelenga kummaliza kisiasa yeye na wale wanaounga Demokrasia ya kweli ndani ya CHADEMA.

Zitto anasema atapambana kuhakikisha anapata haki yake,na atakuwa wa Mwisho kuondoka CHADEMA tena kwa hiali yake.

Mwisho kabisa Mh.Zitto amewaahidi wanakigoma kuwa hatafanya maamuzi yoyote kabla hajarudi tena Nyumbani na kushauriana na wananchi wake.

Amesisitiza kuwa Kigoma ya Leo hii ambayo kila mmoja kwa nafasi yake anajisifia kuitwa mzawa wa kigoma ni moja ya jitihada zake,Pia yeye hayupo kwa Msalahi ya CHADEMA tu,Hoja ya Buzwagi ilikuwa ya Kitaifa,Hoja ya kumuwajibisha waziri Mkuu ilikuwa ya Kitaifa,Lakini hata hii hoja ya PAC ya kukagua mahesabu ya Vyama vya siasa ni ya Kitaifa,Hivyo hayupo tayari kuwamnafiki kwa kuitetea CHADEMA kukaguliwa eti kwa sababu yeye ni Kiongozi ndani ya CHAMA.

Mkutano Umemalizika Salama kabisa,Wananchi wameridhika zaidi na kwa shangwe kwa pamoja wanasema"ZITTO KWANZA,CHADEMA BAADAE"
.


Hakuna kurudi nyuma hadi kieleweke

Vijanaaaaaaaaaaa"nguvu ya Mabadiriko"

Msafara unaendelea ukitokea Ofisi za CHADEMA MKOA hapa Kigoma kuelekea Mwandinga kijijini alikzaliwa Zitto kabwe

Siasa ni Vijana na hii ndio Nguvu ya Umma ilivyojitokeza kumpokea ZItto kabwe hii leo

Vijana wakiwa wamehamasika vya kutosha sana,hapa wanaimba "Kitimtimu utakiona leo,Kwenye nyumba ya Zitto..Slaa umeingiaje"?

Kwa namna msafara ulivyokuwa mkubwa ilimlazimu kila aliyenyumbani kwake kukikimbilia barabarani angalau kupungia mkono kwa Mh.Zitto Kabwe


Ulinzi wa wananchi wenyewe umeimarishwa sana,Vijana wamamrinda Mbunge wao.Kubwa zaidi hakuna askari kwenye msafara huu ni wananchi wanajiongoza na wapo

Zitto Kabwe"Nimerudi nyumbani,Nawasshukuru kwa mapokezi mazuri haya ya Kihistoria hapa Kigoma,Nimerudi Shujaa wenu

Zitto"Asanteni sana,nawapenda sanaa"

Alipokuwa anakaribia kuingia Mwandinga Mh.Zitto kabwe alilazimika kuteremka na kuanza kutembea kuelekea kwenye Mkutano

Msafara bado unaendelea,Wananchi wanasema hakuna kurudi Nyuma mpaka kieleweke

Ni maelfu ya WANANCHI ambao wanatembea kuelekea Mwandinga umbali wa zaidi ya kilomita 15 kwa miguu huku wakiwa na furaha sana ya kukutana na Mbunge wao

Msafara wa magari zaidi ya 100 ukitokea Airpot kumpokea Mh.Zitto kabwe kuelekea Mwandinga,Hapa Shughuli za maendeleo zimesismama kwa muda wananchi wamejumuika kumsindikiza Zitto Mwandinga kuzumngumza na wanakigoma


Ni nyomi ambayo haijawahi kutokea hapa Kigoma

Zitto Kabwe anasema"Nimerudi Nyumbani kuzungumza na nyini kaka,dada,baba na Mama zangu kuhusu maisha yangu ya Kisiasa,Nimerudi Nyumbani kwasababu ndipo nilipokulia na kuanza maisha,Pia nyie ndio mlionifikisha hapa".

Picha inajieleza namna wananchi walivyomiminika Mwandinga kumsikiliza Mtoto wao

Huu ni Upande mmoja wa Sehemu ya Mkutano wananchi wakiwa makini kusikiliza kile Mh.Zitto anaongea kuhusu mwenendo wa Siasa za CHADEMA na namna atakavyokuwa wamwisho kuondoka CHADEMA kwa hiari yake.

Msafara ukiendelea zaidi ya Kilomita 15 kutoa Airport Kuelekea Mwandinga Nyumbani alikozaliwa Zitto Kabwe,Wananchi wamejitokeza kwa wingi sana haijawahi kutokea.
\

Mh.Zitto Kabwe akaihutubia Maelfu ya Wananchi katika viwanja vya Mandinga,Kubwa amesisitiza ataendelea kudai Demokrasia ya Kweli ndani ya CHADEMA na inamuuma sana kuona wanaompiga Mishale ni Wanachadema wenzake.
Maelfu ya Wananchi waliojitokeza kwenye Mkutano wa Mh.Zitto kabwe hapa Mwandinga Kijijini kwake alikozaliwa Mkoani Kigoma,Bango linasomeka "ZITTO KAMA MANDELA KASORO JELA"
Chanzo: Jamiiforums

No comments :

Post a Comment