Naibu Mwakilishi Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa mataifa New York, Ramadhani Muombwa Mwinyi (kulia) akiwa pamoja na Viwe Juma, ambae ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya BENKI ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambao ni wadhamin wa timu hiyo wakimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein Siku ya Jumamosi April 26, ndani ya Ubalozi wa Tanzania jiji Washington DC nchini Marekani, ili kujianda kupambana na timu ya Kilimanjaro Stars kwa mchezo wa kuwania Kombe la Muungano.

Katika kilele cha kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Timu ya  Zanzibar Heroes kupokea Jezi kutoa kwa wadhaminini wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambazo jezi hizo zilitolewa na wageni rasmi walihudhuria katika sherehe hizo akiwemo Mh. Mwigulu Nchemba  ambae ni Mbunge na naibu waziri wa fedha na Uchumi Tanzania bara na upande wa Zanzibar pamoja na Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame mwakilishi na waziri wa nchi ofisi ya rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar.  

Viongozi: Wageni rasmi wa sherehe za Muungano  Mhe: Mwigulu Nchemba (wapili kulia) akifuatiwa na Balozi Mulamula, pamoja na Balozi wa Waziri wa Nchi Zanzibar, Ofisi ya Rais na MBM Dr. Mwinyihaji Makame, (wakwanza kulia) Viwe Juma,wapili kulia  ambae ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein katika Sherehe za Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC.

Wasimamizi wa timu ya Zanzibar Heroes Seif Ameir na Dedie Rouba wakionyesha jezi walizodhaminiwa na (PBZ) Benki ya Watu wa Zanzibar.

Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Viwe  Juma akipata picha ya pamoja na Miss Tanzania USA

Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Viwe  Juma akipata picha ya pamoja na wanamitindo wa Mitindo Night.

Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Asociation Bwana Omari Ali akipata picha ya pamoja na mgeni ndani ya Ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC Nchini Marekani

  

Miss Tanzania USA  akipata picha ya pamoja na  wanamitindo wa Mitindo Night