dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 30, 2014

Ukawa ruksa kuunguruma leo Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.PICHA|MAKTABA 
Na Ibrahim Yamola, Mwananchi

Posted  Jumatano,Aprili30  2014  saa 24:0 AM
KWA UFUPI
“Tunakwenda kuwaelimisha wananchi nini maana ya Katiba, jinsi ya kulinda maoni yao waliyoyatoa yasichakachuliwe na kuwaeleza kwa nini tuliamua kutoka bungeni,” alisema
Dar es Salaam. Hatimaye mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata baraka za polisi.
Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Aprili 19, mwaka huu lakini ukazuiwa na polisi kwa maelezo kuwa intelijensia yao ilionyesha kuwa kungekuwa na tishio la maisha ya watu. Hivyo walishauriwa wapange tarehe nyingine baada ya Sikukuu ya Pasaka.
Hata Aprili 23 ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwa mkutano huo, ilikataliwa na polisi kwa madai kwamba askari na maofisa wa jeshi hilo walikuwa Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yaliyofanyika Aprili 26, mwaka huu.
Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina amethibitisha kuruhusiwa kwa mkutano huo na kuwataka wananchi watakaohudhuria kuwa watulivu kabla na baada ya mkutano.
“Tumewaruhusu kufanya mkutano huo lakini maandamano hayataruhusiwa kufanyika,” alisema Mhina.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema mkutano huo utakaoanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, utahudhuriwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Freeman Mbowe na Dk Willibrod Slaa wa Chadema, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Dk Emmanuel Makaidi wa NLD.
Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wawakilishi 10 kutoka kundi la 201 na wanachama mbalimbali kutoka umoja huo.
“Tunakwenda kuwaelimisha wananchi nini maana ya Katiba, jinsi ya kulinda maoni yao waliyoyatoa yasichakachuliwe na kuwaeleza kwa nini tuliamua kutoka bungeni,” alisema Mtatiro na kuongeza:
“Kesho (leo) tunafanya mkutano Unguja na keshokutwa (kesho) Pemba na tutatoa ratiba ya mikutano mbalimbali itakayofanyika Tanzania Bara kwa makundi tofauti.” Aprili 16 mwaka huu, Ukawa wakiongozwa na Profesa Lipumba walisusia Bunge la Katiba na kutoka nje kwa madai ya kutokuridhishwa na mienendo ya mjadala ya Bunge hilo.
Baada ya kutoka bungeni, walitangaza kufanya mikutano nchi nzima wakianzia Zanzibar.
.
http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Ukawa-ruksa-kuunguruma-leo-Zanzibar/-/1597296/2298354/-/k6yseb/-/index.html

No comments :

Post a Comment