dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 15, 2014

Ardhi, uraia pacha gumzo bungeni

Na Benedict Liwenga, Maelezo
Masuala ya migogoro ya ardhi inayowahusisha wafugaji na wakulima na uraia pacha, yamerejea tena katika mjadala wa katiba mpya unaoendelea Dodoma.

Masuala mengine yaliyochukua nafasi ni haki ya afya, haki ya kuishi ikiwemo sheria ya kunyonga, haki za binadamu, haki ya mtuhumiwa na mfungwa, haki za wafanyakazi na ajira pamoja umri katika ajira pamoja haki za vijana.

Mjumbe wa kamati namba sita,Zaina Madabida, alisema ni vyema kuwepo kwa kipengele kinachotambua mila na desturi za makundi ya wafugaji na wakulima ili kuondoa migogoro ya ardhi ambayo inajitokeza mara kwa mara.

Kuhusu haki ya kuishi pamoja na sheria ya kunyonga, alisema sheria ya kunyonga ni vyema iendelee kuwepo katika kikatiba.

“Adhabu ya kifo iendelee kuwepo kama katiba yetu ya sasa inavyosema kwani kuna watu wao wamekuwa na tabia za kuwaua wenzao,” alisema.

Kuhusu haki za binadamu, alisema maoni ya wachache yamefafanua kuwa haki ya kuishi ianzie tangu pale mimba inapotungwa kwani siku hizi watu wengi wamekuwa na utaalamu katika kutambua viumbe vilivyomo tumboni.Alisema ibara ya 39 inayohusu haki ya mtuhumiwa na mfungwa, kamati yake imeitaka katiba izingatie mazingira rafiki kwa watuhumiwa wenye ulemavu.
Mjumbe wa kamati namba 10, Monica Sophu, alisema masuala ya ardhi yamekuwa na changamoto nyingi na ni vyema ikaundwa Tume Huru ya Ardhi ambayo itakuwa na kazi ya kushughulikia migogoro hiyo.

Kuhusu haki za vijana, mjumbe Jesca Msavatavangu, alisema haki hizo hazijaainishwa vyema na kushauri katiba iainishe haki zaote za vijana.

Kuhusu uraia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alisema sura ya 56 inayohusu suala la uraia ni vyema likaangaliwa kwa umakini mkubwa.

Aidha alipendekeza uraia wan chi moja kwa sababu Tanzania bado haijaweza kujilinda vya kutosha.

“Watu watatumia fursa ya uraia pacha kuhujumu uchumi wetu, kwani kuna mazingira mengi ya rushwa, hivyo suala la hili lije kufikiriwa baadaye sana sio sasa hivi,” alisema.

No comments :

Post a Comment