- ATUPIGIA SIMU ZANZIBAR ETI KUTUSUTA KUWA HAJAFA BADO!
- ATUTISHIA KAMA TUNAZIWEZA TUMFUATE DSM!
Mzee Majuto anaonekana akiongea na Zanzibar Ni Kwetu jana jioni kutoka kwake mjini Dar-Es-Salaam!
Jana
blog letu la Zanzibar Ni Kwetu liliripoti juu ya muvi mpya ya yule msanii mkongwe na machachari wa hapa nchini Tanzania ajulikanae kama Mzee Majuto. Muvi hio ambayo tayari ipo madukani ali-act yeye na Bi Chau. Katika
muvi hii (kwa wale ambao bado hawajaiona)
Mzee Majuto anakufa ghafla ofisini kwake mjini DSM kutokana na kusikia kuwa Bi Chau kafariki baada
ya ajali mbaya iliyotokea huko Sinza wakati akielekea kwao Nyanjati.
Ni kweli kabisa jamani kuwa kila mtu hapendi kufa, hata akiwa ameshakula
chumvi kiasi gani, kwasababu hatufahamu kwanini Mzee Majuto akaacha kazi zake
muhimu na akatupigia simu Zanzibar na huku akifoka kama vile tumemtabiria kifo cha kweli mzee
wetu mpenzi, wakati yeye mwenyewe ndio aliyoiandika hio script ya muvi yake.
Tunahakika kuwa hakuna atakaeamini hii habari ifuatayo, ambayo labda ingelipata kichwa cha maneno kama vile - A fatal head-on collision with King Majuto!
Ilikuwa saa tisa na dakika kama tano hivi ya jioni hio jana (Wednesday) wakati
simu ilivyolia. Kupokelewa Mzee Majuta
kwa sauti ya juu akauliza hata bila ya salaam kuwa ni nani huyu Zanzibar
Ni Kwetu? Aliepokea simu akamuuliza, “ kwani wewe mwenzetu ni nani na unamtaka
nani?”. Akasema mimi ni Amri Athumani au kwa jina jengine Majuto. Kusikia hivyo
aliepokea simu akajua kuwa sasa trouble is on the way na
mbio mbio akaipeleka simu kwa Mkuu wa Mawasiliano wa Zanzibar Ni Kwetu, ambae akamuuliza mzee Majuto baada ya
kumuamkia “ tukusaidie nini King Majuto?”.
Mzee wetu Majuto akajibu kwa ghadhabu kubwa sana, “sina haja ya shikamoo zenu,
kwasababu nyinyi ni wauwaji”, na akaendelea kumuuliza tena Mkuu wa Mawasiliano, “ni nani
huyu Zanzibar Ni Kwetu?”. Akajibiwa kuwa huyu sio mtu bali ni blog.
Mzee Majuto akaulizwa umeipata vipi nambari ya simu wakati haipo kwenye blog?
Majuto akajibu,” kwani mimi sijui ku-guguli?”
Akaendelea mzee Majuto…” Kwanini
mnanitakia kifo? Hata wife wangu alishituka alipoona kichwa chenu cha habari kuwa MAJUTO
AMERFARIKI GHAFLA kwenye hilo bologu lenu na mpaka sasa yupo kwenye mshituko bado. Basi mjue mtatangulia nyinyi kwanza mbele ya haki!”. Akaulizwa, "kwani mzee Majuto kwenye
hii muvi yako ya sasa sio ume-act kama ulikufa au vipi? Sasa sisi tulichoripoti kwa wasomaji wetu ni hicho tu
bila ya kuengeza kitu zaidi".
Akaruka mzee Majuto, “ kwanini mmeigeuza hali kama vile kweli nilikufa
wakati ilikuwa ni kwenye muvi tu? Mnajua simu ngapi nilipigiwa leo na wapenzi
wangu wakiniulizia? Siku yangu ya leo yote mmeiharibu”. Akajibiwa kuwa, “kufa
ni kufa tu mzee Majuto, kama kwenye mchezo au nje ya mchezo. Uki-act umekufa
itabidi tuandike hivyo hivyo. Vyenginevyo usi-act umekufa. Sasa ulitaka tueleze
kuwa kwenye hii muvi yako ulikuwa hujafa ghafla kutokana na mapenzi yako juu ya
Bi Chau?”.
Maneno hayo inaonesha yalimkera sana mzee Majuto na ghafla akaruka, “Sikilizeni
nyinyi watoto wa hilo bologu la Zanzibar Ni Kwetu, nyinyi sasa najua kuwa mlikusudia ugomvi na mimi, lakini kama
mnaziweza basi njooni Dalesalama wakati wowote ule na hata nikiwa usingizini hamtonishinda
mimi”, akamalizia mzee Majuto.
Mzee Majuto akaelezwa kuwa hakuna ugomvi na wala hapajakusudiwa shari na
kama anahisi hivyo basi anaombwa radhi. Mwisho mzee Majuto akaulizwa, “ je,
tunaweza kupata discount ya bei ya video cassette moja kwaajili ya maktaba
yetu?” Mzee Majuto akaruka kwa sauti kali na kusema, “kwa nyinyi Zanzibar Ni
Kwetu bei ni laki moja” na akaikata simu hapo hapo!
Pia soma: http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2014/11/mzee-majuto-kifo-chake-cha-ghafla.html
Pia soma: http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2014/11/mzee-majuto-kifo-chake-cha-ghafla.html

No comments :
Post a Comment