Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 3, 2014

Warioba awasuta kwa Nyerere, vurugu zaibuka

Aliyekuwa Mwenyekiti wa  Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu,  Jaji Joseph Sinde Warioba akitolewa nje ya ukumbi wa Ubungo Plaza akiwa na ulinzi mkali baada ya kutokea fujo katika kongamano lililofanyika jana.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba akitolewa nje ya ukumbi wa Ubungo Plaza akiwa na ulinzi mkali baada ya kutokea fujo katika kongamano lililofanyika jana.
Dar es Salaam. Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Sinde Warioba jana alivamiwa na kikundi cha watu wachache waliohudhuria mdahalo wa Katiba wakati akihoji vitendo vya baadhi ya watu kutumia vibaya jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Jaji Warioba, ambaye alikuwa msemaji mkuu kwenye mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alikuwa akihitimisha hotuba yakle aliyoianza saa 9:15 alasiri, kwa kuhoji kuhusu watu wanaotumia vibaya jina la Mwalimu Nyerere kupitisha hoja zao katika misingi isiyokubalika.
Vurugu hizo zilidumu kwa takriban dakika 45 ndani ya ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Blue Pearl, Ubungo lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida wasaidizi wa waziri huyo mkuu wa zamani, walimtoa ukumbini dakika 30 baada ya sakata hilo kuanza, hali iliyowapa nafasi vijana hao walionekana kujiandaa kufanya vurugu, kumsogelea na kumpiga.
Baadhi ya watu walionekana kumzonga Jaji Warioba ambaye alikuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ni pamoja na aliyekuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Paul Makonda. Baada ya tukio hilo, polisi waliokuwa na silaha na wakiwa wamevalia nguo za kiraia walimtoa Jaji Warioba ukumbini.
Makonda na Amon Mpanju, ambaye pia alikuwa mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, nao waliokolewa na polisi kutokana na vijana walioonekana kumuunga mkono Jaji Warioba kuwatuhumu kuhusika kwenye vurugu. Makonda aliambulia kipigo na kulazimika kujificha katika moja ya ofisi zilizopo hotelini hapo.
Mbali na Jaji Warioba, wajumbe wenzake wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambao ni Humphrey Polepole, Profesa Paramagamba Kabudi, Profesa Mwesiga Baregu, Awadhi Said na Ester Mkuchu nao walitolewa kwenye ukumbi huo na kupelekwa katika chumba maalum hotelini hapo.
Akitolea mfano watu wanaotumia vibaya jina la Mwalimu Nyerere kiasi cha kuwashangaza hata wale waliowahi kuishi naye kwa karibu, Jaji Warioba alihoji iwapo Mwalimu Nyerere angekuwa hai angekubali mambo haya yapite.
Baadhi ya mambo aliyodai kuwa hata Mwalimu Nyerere asingeweza kuyapinga ni miiko ya uongozi, viongozi kupokea zawadi na kuzimiliki.
“Watu walimuandikia barua Mwalimu Nyerere kumshawishi kuwa fedha zake zitakuwa salama kama ataziweka nje ya nchi, siyo kama alikataa tu, alitangaza jambo hilo katika vyombo vya habari,” alisema.
Huku akizungumza kwa mtindo wa kuuliza swali Jaji Warioba alisema: “Nauliza, hivi, Mwalimu Nyerere angekataa miiko ya uongozi isiingizwe katika katiba? Angekubali watu wawe na akaunti nje ya nchi? Watu wapate zawadi wakae nazo? Labda huyo si Mwalimu.”
Jaji Warioba, ambaye alianza kushangiliwa kwa nguvu baada ya kuzungumza mambo hayo, alisema: “Kwa sisi tunaomjua vizuri Mwalimu, tunajua kuwa ndio yuleyule ambaye alilipitia Azimio la Arusha lililokuwa msingi wa utu na kutoona hata sehemu moja yenye makosa ya kurekebisha.”
Mifano hiyo iligeuka ‘mwiba mchungu’ kwa baadhi ya waliohudhuria mdahalo huo ambao walionekana kujiandaa kutokana na kwenda ukumbini hapo na mabango yanayoonyesha kukubali Katiba Inayopendekezwa.

Baada ya mneno hayo, watu hao walisimama na kunyanyua mabango yaliyokuwa yamebeba ujumbe mbalimbali, ukiwemo “Katiba Inayopendekezwa tumeipokea na tumeikubali”.
Kitendo hicho kiliwakera baadhi ya washiriki kwenye mdahalo huo ambao walisimama na kuanza kuwakamata waliokuwa wamebeba mabango hayo na kuanza kuyachana.
Licha ya Jaji Warioba na mshehereshaji wa mdahalo huo, Said Kubenea kuwataka washiriki kutulia, vurugu zilizidi na kudumu kwa dakika 45 huku viti vikirushwa kutoka upande mmoja kwenda mwingine na kusababisha watu kukimbia hovyo.
Wakati washiriki wakikimbilia nje, walikutana na polisi ambao walipiga mabomu ya machozi ya kuwafanya baadhi yao kurejea ndani ya hoteli hiyo.
Baada ya hali kutulia Joseph Butiku, ambaye ni mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, alirudi ukumbini na kueleza kuhuzunishwa na kilichotokea na kufafanua kuwa kutokana na hali ya kiusalama ni vyema mkutano huo ukaahirishwa.
Akizungumza kwa masikitiko, Butiku alisema: “Hata enzi za Nyerere aliwahi kupita katika wakati mgumu. Lakini haikuwahi kufikia hatua ya watu kupigana ngumi na mateke na kurushiana viti kama tuliyoshuhudia hapa. Kutokana na aibu iliyotokea leo, kwa nia njema ya kuzuia lisije tokea jingine zaidi, tunaahirisha mdahalo huu kwa ajili ya kwenda kujipanga vizuri zaidi.”
Butiku alisema anawafahamu baadhi ya watu walioandaa vurugu hizo na kusisitiza kuwa watu wa aina hiyo hawataruhusiwa kushiriki kwenye midahalo hiyo ambayo itaendelea kuwepo katika maeneo mengi ya nchi ili kutoa fursa kwa wananchi kujadili namna ya kupata katiba iliyo bora.
Mpaka gazeti hili linaondoka hotelini hapo, Makonda alikuwa hajatoka eneo ambako inadaiwa alijificha huku Jaji Warioba akiondolewa chini ya ulinzi mkali.
Alipotoka eneo la nje ya hoteli hiyo, Jaji Warioba alikumbana na umati mkubwa wa watu ambao walikuwa wakiimba nyimbo za kumsifu na kumuita kuwa ndio rais ajaye wa Tanzania.
 Kabla ya vurugu.
Shangwe, vifijo na nderemo zilitawala kutoka kwa zaidi ya watu wengi waliohudhuria mdahalo huo wakati Jaji Warioba na wenzake walipokuwa wakiingia ukumbini saa 9:00 alasiri.
Kabla ya Jaji Warioba kuanza kuzungumza katika mdahalo huo ambao pia ulihudhuriwa na makada wa CCM na Chadema, Butiku alisema: “Hayawi hawayi, sasa yamekuwa. Tume imeshamiliza kazi na Bunge nalo lmeshamaliza kazi yake. Lengo ni moja tu, ni maendeleo yetu sote.”
Aliongeza: “Sasa tujadili kwa utulivu kwani hatusimamiwi na makundi na badala yake tunaijadli Katiba kwa sheria, hakuna kutishana, kuogopa mtu wala kusimamiwa na chama na hata shinikizo,”
“Miaka ijayo tusije tukawa kwenye kundi la wajinga na kushindwa kujua tulikuwa tunajadili nini ili tuepuke maswali kutoka kwa wajukuu zetu na watoto pia.’’
 Warioba
Kabla ya Jaji Warioba kuanza kuzungumza, mshehereshaji wa mdahalo huo Hamza Kassongo alimuomba atoe jibu kama ni kweli Katiba Inayopendekezwa imebeba asilimia 80 ya maudhui ya rasimu ya Pili ya Katiba.
Jaji Warioba alianza kwa kuifafanua Sheria ya Kura ya Maoni kuwa inamtaka wiki mbili baada ya rais kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa kuitangaza katika gazeti la Serikali na kuiagiza Tume ya Uchaguzi (NEC) kuanza kusimamia mchakato huo.
Pia alieleza kuwa kazi ya kutoa elimu kwa wananchi itakayofanywa na NEC na asasi za kiraia kwa mujibu wa sheria hiyo inatakiwa kufanyika kwa siku 60, baada ya hapo itafanyika kampeni kwa muda wa mwezi mmoja.
“Sheria inasema Kamati ya Kampeni ndiyo itafanya kampeni. Kamati hizo zinakuwa mbili ambazo ni Kamati ya Kitaifa na ya Jimbo. Kamati moja ni ya kuungaa mkono Katiba Inayopendekezwa na ya pili ni ya kupinga, zote lazima zisajiliwe na NEC. Baada ya kampeni NEC itasimamia upigaji kura, kuhesabu na kutangaza matokeo,” alisema.
Jaji Warioba alikosoa utaratibu wa kufanya maboresho daftari la kudumu la wapigakura na kuonyesha wasiwasi wake kama kura ya maoni itaweza kufanyika kama sheria inavyosema kutokana na kamati kutoundwa na muda wa NEC kuwa mdogo.
 Katiba Inayopendekezwa
Akigusia Katiba Inayopendekezwa, Jaji Warioba alisema kuna baadhi ya mambo ya muhimu yaliyokuwa katika rasimu ya Katiba yameondolewa
“Katiba Inayopendekezwa haijasambazwa ipasavyo. Tunatakiwa kutotazama wingi au uchache wa ibara, tutazame Katiba ina mabadiliko gani,” alisema.
Aliyataja mabadiliko ambayo hayapo katika Katiba ya sasa lakini yalikuwepo kwenye Rasimu kuwa ni tunu na maadili na kusisitiza kuwa mambo hayo yalikuwa mapya.
Pia aligusia kuondolewa kwa madaraka ya wananchi katika Katiba Inayopendekezwa, mawaziri kutokuwa wabunge, madaraka ya rais kutopunguzwa, mgombea binafsi kuwekewa masharti mengi, haki mbalimbali kutodaiwa mahakamani, idadi ya wabunge kuongezwa pamoja na muundo wa muungano kuwa unazidisha kero baada ya kuzipunguza.
 Mabango, wasemavyo washiriki
Baadhi ya vijana waliobeba mabango ya kuunga mkono Katiba Inayopendekezwa walilalamikia vurugu walizofanyiwa ukumbini.
“Wamechana mabango yetu… walichokifanya ni kuzuia uhuru wetu wa kutoa mawazo yetu,” alisema mmoja ya vijana hao aliyejitambulisha kwa jina la John Ndumbaro.
“Warioba anapingana na Katiba Inayopendekezwa, lakini sisi tunaipenda na ndiyo maana tumekuja na ujumbe wa kuielewa, kuipenda na kuikubali.”
Asilimia kubwa ya mabango yalikuwa yanafanana yakiwa na ujumbe wa Katiba Inayopendekezwa tumeielewa, tunaipenda na tunaikubali.
Alipoulizwa iwapo kundi lao ni miongoni mwa wafuasi wanaodhaniwa kutumwa na CCM kuvuruga mdahalo, Ndumbaro alisema nchi inawagusa watu wote na kwamba hawakuwa wafuasi wa chama chochote bali walienda kutetea nchi.

Naye Wagese Wilson alisema kilichotokea pale ulikuwa ni uhuni ambao anaamini ulipangwa na kikundi anachodhani ni cha wana-CCM.
“Kimsingi hizi vurugu ziliandaliwa kwa sababu ulinzi ulikuwepo nje muda wote. Kwa nini baada ya purukushani kutokea zimepita takriban dakika 40 bila polisi kuingia na kumlinda mtu mkubwa kama Warioba?” alihoji.
Mmoja ya washiriki waliokuwa jirani kabisa wakati Warioba akitolewa nje ya ukumbi, William Ndiyekeiya alisema alisikitisha kuona kiongozi mkubwa kama Warioba akikosa ulinzi wa kutosha hasa katika mdahalo wa kitaifa.
“Yule mtu wa CCM alikuwa nyuma ya Warioba huku amemng’ang’ania na askari wa FFU (kikosi cha kutuliza ghasia) aliyekuwa ameingia hakuonyesha hali yoyote ya kutaka kuwatenganisha.
“Hili ni tatizo la serikali la kushindwa kuleta ulinzi mapema…dakika 45 baada ya vurugu ndiyo wanaleta askari ndani! Lazima watambue kuwa Watanzania wa sasa siyo sawa na wale wa mwaka 1977 au 1982,” alisema Ndiyekieya.
Mpango wa Vurugu ulipangwa
Mmoja wa Wanafunzi wa Taasisi ya Maendeleo na Usimamizi wa Maji (WMDI) ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa ajili ya usalama wake, alisema kuwa juzi usiku kulikuwa na ujumbe mfupi uliokuwa ukisambazwa ukitaka kujiandaa na mdahalo.
“Nilipokea ujumbe uliokuwa unatutaka leo muda wa saa 6:30 kuja Ubungo Plaza na nauli zingetolewa… baadaye kidogo ujumbe huo ulieleza kwamba hatukutakiwa kwenda na nguo za kijani wala njano kwa sababu kulikuwa na shughuli maalumu,” kilisema chanzo hicho.
Alipouliza mtu aliyekuwa anawasiliana naye, mwanafunzi huyo wa mwaka wa tatu, alijulishwa kuwa aliyetuma ujumbe alikuwa ni mmoja wa viongozi wa chama kimoja chenye tawi chuoni hapo.
“Pale Chuo hakuna matawi ya vyama vingine…na zitazame meseji zote hizi tulizokuwa tunachati akijaribu kutuelekeza namna ya kuandaa ‘kazi hiyo maalumu’,” alisema.
“Hata baada ya kuingia ukumbini nilianza kuwaona wanafunzi wenzangu kidogokidogo ambao walienda kujirundika upande mmoja na baadaye kuanza kuonyesha mabango,” aliongeza huku akimuonyesha mwandishi wetu meseji hizo.
 Imeandaliwa na Fidelis Butahe, Hussein Issa, Andrew Msechu na Nuzulack Dausen.
Also see:  http://zanzibarnikwetu.blogspot.ca/2014/11/fujo-na-ngumi-kwenye-mdahalo-wa-katiba.html
Comments: 
  • Avatar


    hapo ndo CCm inathibitisha kwa watanzania kuwa katiba pendekezi si kwa ajili ya watanzania ni kwa ajili ya manufaaa ya Chama....watanzania vulugu za jana ni ishara ya urafi na tamaa za CCM


      • Avatar


        Huu ni uhuni tena ni kitendo ambacho hakikubaliki,nahisi ni mpango tuu ulikuwa umepangwa ilikuvuruga shughuli hii ambayo ilikuwa imepangwa na yenye manufaa kwa Taifa kubwa la #Tanzania na #Wananchi wake.
        Haiwezekani jambo kama hili kutokea kiurahisi kiasi hichi na ulinzi ulukuwapo, kama sio mpango ni nini?. #Katiba ni yetu na watu wote kwa ujumla, na hatutaweza kukubaliana na kupokea mambo ambayo hayana tija kwa sisi wananchi, tutazidi kuipigania katiba na kuipinga kabisa Rasimu iliyo yaacha #Maoni yetu sisi na kuweka wanayo fikiria wao.
        Haiwezekani!haiwezekani!haiwezekani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Kila mtu sasa anajitambua na sikama hapo awali tulivyokuwa tukipelekeshwa tuuuu kama #Punda.


          • Avatar


            Warioba hakuwa na lolote la "..kusuta .." alitaka kujipigia na kusaidia upotoshi wa Kisiasa wa Wapinga Mapinduzi na Muungano. Ni kiburi cha kujiamini kuwa asemalo yeye iwe ndio "Bblia au Msahafu". Wabunge wa BMK walikuwa na kila haki na kwa mujibu wa sheria za nchi ".... kuyakubali au kuyaboresha mapendekezo ya timu ya Warioba ... ". Wabunge ndio watunga sheria sio Warioba na wabarabarani wenye chuki kali dhidi ya waliochaguliwa na wengi Bungeni - CCM. Huo ndio ukweli hasa.Vyengine vyote ni porojo la upotoshi wa Akina UKAWA .


              • Avatar


                Kuna jambo moja ambalo twapasa watanzania wote kujifunza. Nguvu ya uvumilivu. Ushujaa wa kimya. Hebu kumbuka shairi la sungura aliyezikosa ndizi alizohitaji kutuliza njaa yake, kisha akaamua kusema, 'sizitaki mbichi hizi.'
                Jana nilikuwa naangalia mjadala ITV na niliona, kwa kadri kamera ya ITV ilivyoonesha mabango yakinyanyuka. Pamoja na kuwa sikuweza kusoma kilichokuwa kwenye mabango lakini ni wazi walioyanyanyua walikuwa na mtizamo tofauti na wengi wa waliokuja kwenye mkutano ule. Kuja kwenye mkutano wenye uelekeo wa mtizamo tofauti na wako si kosa. Je, kunyanyua bango (ama mawasiliano tofauti wakati mkutano ukiendelea, bila ruhusu toka kwenye ratiba?) Hili si ustaarabu. Pengine waweza kuliita kosa. Je, kuwapiga walionyanyua mabango, kuyachana, na kuwatafuta ili kuendelea kuwakwida? Kwa mtazamo wangu hili ndilo kosa kubwa zaidi. Nitaeleza kwanini?
                Aliyeleta bango na kujaribu kulinyanyua kinyume na mkutano amekuja kuvuruga. Pia amekuja kuwashangazeni kuwa ana mtazamo tofauti na mkondo mkuu wa mkutano wenu. Kumpiga, kumtafuta kumkwida kama mwizi ni kumsaidia kutimiza makusudi yake. Tena mnayatimiza kuliko hata kiwango alichotarajia kwani hatimaye neno vurugu limetumika kuelezea, mdahalo.
                Laiti kama ingetumika nguvu ya uvumilivu na ukimya. Mabango yangenyanyuliwa juu, juu, juu. Wasemaji wangeendelea kusema na kuendelea kama vile hakuna kinachoendelea, kisha naamini ingefikia wakati wenye mabango wangeyashusha. Ama, ingekuwa rahisi kuwaambia, ujumbe wenu umeshaonekana, tunaomba myashushe. Pengine, hata simu zingepigwa kwa vyombo vya usalama baada ya dakika 60 tangu wanyanyue mabango. Kisha tungeone vyombo vya usalama vikiwataka walioshika mabango kuyashusha ama kutoka ukumbini kwa kuwa mabango yao hayako kwenye ratiba ya mkutano.
                Kitendo cha kuyachana, kinanirudisha kuwaza vile ambavyo siku zote naogopa kudhania. Kwamba bado tuna madikteta wengi miongoni mwetu. Bado hatuwezi kuvumilia kusikia sauti ikisema kinyume chetu, bado, bila kujali tuko madarakani ama ukabwelani, tunataka kusikia na kuona tu kile tunachokiamini. Bado ndani ya utamaduni wetu hatuko tayari kuulizwa swali rahisi, KWANINI? ama, NINA WAZO TOFAUTI KABISA LA LAKO.
                Ningeulizwa kushauri nini kifanyike kwenye mikutano ya aina hii mbeleni ningesema hivi. Maneno kama ya Mh. Butiku, yapewe misisitizo kivitendo kabla ya mjadala kuanza. Mh. Butiku alisema mwanzoni kuwa, 'atakayekusukuma...." Natamani kuona katika mikutano ya aina hii mbeleni na katika kampeni zitakazokuja baadaye kuwepo na kipindi cha dakika 10 cha kueleweshana na kujaribu kuigiza (role playing) nini cha kufanya pale anapokuja mtu na mawasiliano (maneno, picha, bango, kelele) tofauti na matarajio ya wengi. Apigwe, achaniwe mawasiliano yake, aminywe, atukanwe, apewe nafasi kinyume cha ratiba, ama afanyiweje? Halafu watu wakishajua nini cha kufanya, basi mkutano uendelee.
                Nayaogopa maneno ya Mh. Butiku kuwa watu wa namna ile ya jana hawataruhusiwa kwenye mikutano ijayo. Kauli hiyo inaweza kutafsiriwa vibaya na wengine kumaanisha kuwa wakionekana waminywe. Na kama ni hivyo itakuwa ni gharama nafuu sana kuvuruga kila mkutano ambao vinginevyo una makusudi thabiti na makini kama ule wa jana.
                Badala ya kuwazuia, ni bora kuinua mawazo na mtizamo wa washiriki wa mdahalo kuwa juu juu juu zaidi ya vijibango hamsini, au hata mia vilivyopangwa kuja kuvuruga. Waache wanyanyue mabango, waitieni vyombo vya dola ndio vije kuwashughulikia, si vije kuwasaidieni kutoka nje katika mahali ambapo nyie ndio wenyeji.
                Najua ipo siku utamaduni wetu wa shikamoo utafika mahali hapo. Nimeweka kifungu maneno utamaduni wa shikamoo kwa kuwa najua kabisa kuna ambao waliwaka jazba kwa kushangazwa inakuwaje vijana wanamkosea 'heshima' mtu kama Warioba akiwa jukwaani. Huo ndio utamaduni wetu, mkubwa akiongea wadogo (wa umri, exposure, elimu, wasio wenyeji, etc) wakae kimya. Katika kujenga uvumilivu wa mitazamo tofauti wakati mwingine kanuni za kitamaduni zetu zitalazimika kuchunua kiti cha nyuma. Na ndivyo ilivyo: kwani waliokuwa Dodoma wangeangalia hilo wangechakata muswada kiasi kile, si 'wangeheshimu' ulikotoka?
                Hatimaye, neno la mwisho, tafadhali kila mkutano wa katiba unapofanyika rasmi, kiwepo kipindi cha dk 10-20 kuweka ground rules zitakazofuatwa na kila mtu katika kushughulika na mitizamo tofauti na ya kwake ama inayoonekana kuwa ya wengi kwenye kusanyiko. Maisha matamu.


                  • Avatar


                    Mwananchi andikeni maoni ya Watanzania. Mimi nataka niwaambie viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya shina hadi juu. Mnafikiri kile alichokipata Makonda ni kipigo, la hasha hiyo ni trela tu. Kapigo cha CCM mtakipata kwenye kupigia Katiba kura na kwenye uchaguzi. Mumewanyima watoto mikopo mkafiche fedha nje yaq nchi ni akili hiyo. Wakenya kuja kukaa na kufanya kazi Tanzania wametusaidia sana kujua haki zetu. Watanzania tulikuwa hatujui haki zetu kabisa. CCM imewafanya Watanzania kuwa vijakazi wao. Wanataka kila kitu tuseme ndio kama wabunge wao. Wale vijana waliomletea fujo Warioba wametumwa na kulipwa shilingi 10,000/= kila mmoja na CCM. Wale ni watu tunawajua tunawaita "WACHUMIA TUMBO". Huwezi kupanda jukwaqani kutaka au kumpiga Warioba kama hujatumwa. Siku zote watu wanaolipwa na CCM kufanya hata fujo kwenye mikutano ya UKAWA ni hawa hawa "WACHUMIA TUMBO". Mimi niwaambie utafika mwisho wenu siku sio nyingi. CCM mkileta mchezo tutamuweka Mh. SINDE WARIOBA agombee Urais kwa tiketi ya UKAWA.


                      • Avatar


                        Demokrasia maana yake ni kuwa na uhuru wa mawazo hata kama mawazo hayo
                        wewe huyapendi. Demokrasia inasisitiza kuvumiliana panapokuwepo tofauti
                        ya mawazo.
                        Sasa kulikuwa na tatizo gani kwa baadhi ya washiliki
                        wa huo mdahalo kuonyesha mabongo ambayo yalikuwa yanapingana na mawazo
                        ya msemaji kutoka jukwaa kuu? Kwanini waanze kurushiwa viti baada ya
                        kuonyesha mabango? Ina maana kwa mujibu wa washiriki wengi wa mdahalo
                        huo wao walitaka kila mshiriki apige makofi kwa yote aliyosema
                        Mwanaharakati Warioba?
                        Mbona kwenye mikutano ya viongozi wengi
                        tu wa Serikali akiwamo hata Rais wakati anahutubia hujitokeza watu
                        wakiwa na mabango tofauti na ujumbe wa hotuba, lakini hatujawahi kuona
                        wakitimuliwa na au hata kupigwa kama ilivyokuwa kwenye mdahalo wa
                        Warioba?
                        Wafuasi wa Warioba mnataka kila anachosema Warioba
                        kisipingwe hadharani? Kama ni hivyo basi hiyo siyo demokrasia.
                        Demokrasia ya namna hiyo tunajua iko CHADEMA (CHAgga DEvelopment
                        MAnifesto) tu. Huko ndiko kila anachosema Mbowe na Babu Slaa Kuwa na
                        Huwa.
                        Wapenda amani Tanzania tunalaani vikali kabisa kitendo
                        hicho cha kuwashambulia washiriki wa mdahalo walioonyesha mabango ya
                        kupinga maneno ya Warioba, kwani mdahalo huo ulikuwa ni wa wazi na watu
                        wote walikaribishwa, na wala haukusema kuwa wale wenye mawazo tofauti na
                        ya Warioba wasihudhurie. Ungelikuwa umesemwa hivyo na halafu hawa
                        wanaoitwa eti wahuni wamefanya vurugu wakahudhuria basi kweli hapo
                        tulikuwa na haki ya kuwalaani nao vikali.
                        Lakini kwa hili
                        Warioba na wafuasi wako hamuwezi kuzikwepa lawama hizi. Warioba Usifanye
                        siasa kwa kutumia mlango wa nyuma. Kufanya hivyo ni u coward na unafiki
                        mkubwa ambao haustahili kufanywa na mtu kama wewe uliyekuwa na heshima
                        kubwa hapa nchini ambayo sasa umeichafua kabisa hadi kwenye sifuri.
                        Nenda kashirikiane waziwazi na wenzako UKAWA/UKIWA katika harakati zenu.
                        Usituharibie nchi yetu sisi vijana. Wewe jua limeshazama na ulikaa kwa
                        amani muda wote huo sasa iweje wewe utake kutuharibia amani yetu?
                        MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU ENDELEA KUMUANGAMIZA WARIOBA NA KUNDI LAKE KWA AJILI USALAMA WA NCHI YETU TUKUFU.

                      No comments :

                      Post a Comment