Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 27, 2014

Chenge, Ngeleja, kuadhibiwa ndani ya siku 21 zijazo

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti bungeni, Andrew Chenge.

Na Ibrahim Yamola, Mwananchi

KWA UFUPI
Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema jana kuwa utekelezaji wa maazimio ya Bunge kwa upande wa mhimili huo wa dola utafanyiwa kazi mapema mwakani.

Dar es Salaam. Wenyeviti watatu wa Kamati za Bunge waliopendekezwa kuwajibishwa na Bunge hilo katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow wataondolewa katika nyadhifa zao ndani ya siku 21 zijazo, imeelezwa.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema jana kuwa utekelezaji wa maazimio ya Bunge kwa upande wa mhimili huo wa dola utafanyiwa kazi mapema mwakani.

“Hilo litatekelezwa wakati wa Kamati za Bunge ambazo zitaanza mwishoni mwa wiki ya pili ya Januari mwakani kwa kamati husika kuchagua wenyeviti wapya.”

Wenyeviti hao ni wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, William Ngeleja wa Katiba, Sheria na Utawala na Andrew Chenge wa Kamati ya Bajeti.

Tuhuma zao.
Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi (CCM) alitajwa katika ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa aliwekewa Sh1.6 bilioni katika akaunti yake binafsi kama ilivyokuwa kwa Ngejela (Sengerema -CCM) ambaye aliingiziwa Sh40.4 milioni.
Wote waliingiziwa fedha hizo na mmiliki wa Kampuni ya VIP Engineering & Marketing, James Rugemalira.

Mwambalaswa, ambaye pia ni Mbunge wa Lupa (CCM), ametajwa kwa kuwa alikuwa makamu mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco ambayo Bunge liliazimia kuwa wajumbe wake wawajibishwe.

Katika azimio namba tatu, Bunge lilielekeza kuwa kamati husika za kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao wenyeviti tajwa wa kamati husika za kudumu za Bunge.

Utekelezaji wa azimio hilo unakuja baada ya Serikali kuanza kuwawajibisha vigogo wake waliotajwa katika ripoti hiyo.

Jumatatu iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alimfukuza kazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye kama ilivyokuwa kwa Chenge na Ngeleja, aliingiziwa Sh1.6 bilioni katika akaunti yake binafsi kinyume na kanuni za maadili ya viongozi wa umma.

Pia, wakati Rais Kikwete akimuweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, juzi Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alimsimamisha kazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake.

Hao wote walitanguliwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ambaye alijiuzulu kutokana na kashfa hiyo akisema ushauri wake haukueleweka hivyo kuchafua hali ya hewa.

  • Avatar








    Ikulu mambo yanaborongwa mno,uchunguzi ulishafanyika,sasa rais anatuambia anasubiri uchunguzi mwingine upi huo?nini cha maana atakileta kwa wazee wa Dsm tena kurudia rudia kile ambacho bunge limeshakifanyia kazi,uswahili wa kikwete unanitia kichefuchefu,unajaribu kuwafanya watu waone kuwa unawahoji,wahalifu wako,wakati kila kitu kipo wazi,sasa wewe unachukua njia ndefu ya nini.wewe kama rais,mawaziri wote waliohusishwa na kasfa hiyo ungewaambia unawawajibisha wapishe uchunguzi wa haki ufanyike,unashindwa kuwawajibisha mawaziri,je wabunge waanze na wewe umalizie?kina vichenji bado sana wanatakakuwa na benk zao labda wataridhika walau kidogo,mbona hiyo nichenji tu kwa change jamani!ninaudhika na mambo ya rais ya uswahili na kulindanana.








      • Avatar








        Chenge na Ngeleja hata wakinyogwa mimi sitasikitika. Hawa ndio wameifikisha Tanzania hapa tulipo. Serekali imefilisika hata kununua Aspirini haiwezi. Waginjwa wanafia magetini shauri ya uongozi mbovu wa CCM. Kuanzia chini mpaka juu hakuna mwenye afadhali. Bomu tunasubiri lilipuke wapelekwe mahakama ya ICC. Holi halikwepeki tunasubiri waweke vyeo vyao chini seke seke lianze. .








          • Avatar








            kuwavua uenyekiti is nothing tunachotaka wafikishwe mahakamani kwa kuliibia taifa








              • Avatar








                BUNGE GANI HILO LA MAKABWELA








                  • Avatar








                    Ni kuvuliwa madaraka tu? Hamna kupelekwa mahakamani? Mbona Mramba ana kesi ya kutumia madaraka vibaya na kusababisha serikali hasara? Kama hamna kesi dhidi yao,hayo maamuzi /maazimio ya bunge ni bure tu.








                      • Avatar








                        Huyu bwana chenge atahusika na kashfa ngapi ili achukuliwe hatua madhubuti?








                          • Avatar








                            Ni nchi zenye mfumo wa kifisadi tu ambazo kiongozi wa umma hata apewe mabilioni ya fedha na wafanyabiashara bila sababu ya msingi, ili mradi fedha zile siyo za wizi, mpokeaji haulizwi, sana sana serikali inaweza kumuongeza cheo. Maadili yako wapi. Wakati bunge limekomaa kuhakikisha maazimio yake kuhusu sakata la escrow yanatekelezwa na serikali, bunge lenyewe limeshindwa kutekeleza maazimio yake lenyewe yanayohusu wabunge. Navishangaa pia vyombo vya habari, viko kimya katika kufuatilia viongozi wa umma waliojazwa mapesa bila maelezo, Kiongozi anawekewa zaidi ya 40,000,000/- katika akaunti yake lakini hakuna anayejali, mwingine anawekewa 200,000,000/- bila maelezo, haulizwi, kiongozi wa umma anawekewa 400,000,000/- haulizwi, kiongozi anawekewa 1,600,000,000/- bila maelezo, haulizwi, lakini tunaambiwa eti kuna tume ya maadili ya viongozi wa umma, ni maadili gani hayo.









                            No comments :

                            Post a Comment