Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 28, 2014

WAZANZIBARI WAMJIA JUU JK. WAMTAKA AZIDAI PESA ZILIZOPORWA NA WEZI WAPELEKWE MAHAKAMANI!!!

OOOOOOOO

Watuhumiwa wa escrow wabanwa mbavu Zanzibar 
Anna Tibaijuka and Mzee Vijisenti are the Chief culprits!

Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi

KWA UFUPI
Msimamo huo umetolewa na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) na Taasisi ya Utafiti na Sera za Kijamii Zanzibar (ZIRPP) baada ya waliotajwa katika sakata la escrow kung’oka na mmoja kusimamishwa kazi.

Zanzibar. Taasisi za kutetea haki za binadamu na kusimamia misingi ya Utawala Bora Zanzibar zimesema viongozi waliohusishwa na ufisadi wa Sh 306 bilioni kupitia Akaunti ya Tegeta Escrow wakamatwe na kufikishwa mahakamni badala ya kufukuzwa kazi peke.

Msimamo huo umetolewa na Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) na Taasisi ya Utafiti na Sera za Kijamii Zanzibar (ZIRPP) baada ya waliotajwa katika sakata la escrow kung’oka na mmoja kusimamishwa kazi.

Rais wa ZLS, Awadhi Ali Said alisema viongozi waliohusika haitoshi kujiuzulu bila ya kufunguliwa mashtaka kwa vile kuna makosa ya jinai yamefanyika katika kashfa hiyo.

Alisema viongozi walioonyesha udhaifu wa kiutendaji na uzembe hadi kusababisha fedha hizo kuiibiwa wanapaswa kujiuzulu kulinda misingi ya uwajibikaji wa pamojahata kama hawakuhusika moja kwa moja katika uchotaji wa fedha hizo.

Hata hivyo, alisema kazi ya kupambana na rushwa na ufisadi itaendelea kuwa ngumu kama jamii itaendelea na tabia ya kuwapokea kama mashujaa viongozi wanaofukuzwa katika nyadhifa zao kutokana na kuhusishwa na kashfa za ufisadi.

Pia, alisema kwamba ZLS inaamini kuwa katika uwajibikaji wa pamoja Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatakiwa kujiuzulu.

Mkurugenzi Mtendaji wa (ZIRPP) Muhammed Yussuf Mshamba alisema kulingana Ripoti ya CAG, Gavana wa Benki Kuu na Waziri wa Fedha wanapaswa kujiuzulu ili kulinda misingi ya uwajibikaji wa pamoja.

“Tukisimama katika misingi ya uwajibikaji wa pamoja Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Gavana wa BOT na Waziri wa Fedha waondoke kulinda heshima zao na kupunguza machungu ya wananchi,” alisema Mshamba. Alisema fedha zilizopotea ni fedha za umma kwa sababu Tanesco ndiyo walikuwa wakikusanya tozo.


http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Watuhumiwa-wa-escrow-wabanwa/-/1597296/2571054/-/7xykx2z/-/index.html
.

No comments :

Post a Comment