Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, May 12, 2015

Sadaqatun Jaariyah yako inahitajika Msikiti wa Sogea

  


Msikiti wa Sogea uliopo jirani na Branchi ya Sogea unawaomba na kuwakumbusha Waislamu popote mlipo katika ulimwengu huu wa Arrahmaan kuungana nao tena katika kuwapatia msaada ili uweze kuweka jamvi (Zege) la ghorofa ya kwanza (concrete ceiling) pamoja na kumalizia ujenzi kwa ghorofa ya kwanza.

Alhamdulillaah wamejitokeza wafadhili watakaojitolea kuchangia vitu kama saruji, mchanga, kokoto pamoja na linki.

Hata hivyo wamekwama kwenye upatikanaji wa nondo ambazo baada ya kufuatilia gharama zake, zitagharimu kiasi cha milioni nane.

Nondo hizi wameahidiwa kuzipata endapo watapeleka pesa angalau nusu ili ujenzi uweze kuanza.

Sababu ya kuamua kupanua msikiti ni kwamba kila Ijumaa watu hujaa hadi kuswali nje ambako ni barabara kuu kwani ni hatari kwa magari na wapita njia. Tunamuomba Allaah Subhaanahu Wata'ala atunusuru na ajali.

Tafadhali tunakuomba ujitahidi kwa uwezo wako wote wewe mwenyewe kwanza na uwaombe Waislamu wengine ili tuweze kuumaliza kwa muda mfupi kabisa.

Allaah Subhaanahu Wata'ala anatukumbusha katika Qur'aan "Na kheri yoyote mtakayoitanguliza kwa ajili yenu basi mtaikuta mbele ya Allaah itakuwa kheri kubwa na (yenye) ujira mkubwa" Suuratul Muzammil

Kwa maelezo zaidi na vipi kuwasilisha sadaka yako, wasiliana na Imaam wa Msikiti wa Sogea Sheikh Suleiman Bin Daaud +255 777 460 056

Tafadhali mpelekee ujumbe huu kila mtu, mkono kwa mkono mpaka Peponi.

Baaraka Llaahu fiykum

No comments :

Post a Comment