dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, May 22, 2015

Spika amzuia Kafulila bomu lingine Escrow.

Spika wa Bunge, Anne Makinda.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, amemzuia Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kujibu swali la Mbunge Kigoma Kaskazini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), aliyehoji kwa nini mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Habinder Seth Singh, anaendelea kulipwa na Tanesco Sh. bilioni tano kila mwezi licha ya azimio la bunge.
 
Kafulila alisema: “Bado Seth anaendelea kulipwa Sh. bilioni tano (capacity charge) kila mwezi.”
 
Alisema moja ya maamizio ya bunge ilitaka mmiliki huyo asilipwe fedha hizo.
 
Kabla ya Waziri Mkuu Pinda kuanza kujibu, Spika Anne alisema: “Hili swali ni jipya kabisa, naomba Waziri Mkuu usilijibu.” Baadaye alimwita mbunge mwingine kuuliza swali.
 
Pia alieleza kwamba katika hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwezeshaji (ICSID), ilitaka Tanesco kutolipa kiasi hicho cha fedha, lakini mpaka sasa bado Seth anaendelea kulipwa Sh. bilioni tano kila mwezi.Kafulila aliuliza swali hilo ikiwa ni swali la nyongeza kufuatia lile alilouliza awali kuhusu taasisi ya Serikali ya Marekani inayotoa misaada kwa nchi zinazoendelea (MCC) kusitisha kutoa msaada wa fedha baada ya mwaka jana kufanya hivyo kwa kutangaza kutotoa Dola za Marekani milioni 700 kwa Tanzania kutokana na sakata la akaunti ya Tegeta Escrow.
 
Alisema Waziri wa Fedha alilidanganya Bunge kwa kusema taasisi hiyo haijasitisha kutoa fedha kwa Tanzania kutokana na sakata hilo.
 
Lakini alisema Katibu Mkuu wa wizara hiyo hiyo, alitoa taarifa baadaye akisema taasisi hiyo imesitisha kutoa fedha ilizokusudia sababu kubwa ikiwa ni sakata la escrow.
 
Kafulila alitaka kujua msimamo wa serikali kuhusu uwongo uliotolewa na Waziri wa Fedha.
 
Akijibu Waziri Mkuu Pinda alisema; “Mbunge anataka nitoe msimamo kuhusu uwongo aliotoa waziri wangu…hili si la kwangu ni la Bunge.”
 
Kuhusu tatizo la bajeti ya maendeleo toka kwa wahisani, alisema limekuwa likitokea kwa kipindi cha miaka minne sasa na sio kwa sababu ya sakata la akaunti ya escrow.
 
“Kwa miaka minne mfululizo wadau wa maendeleo hawajatoa fedha zote na sio kwa sababu hiyo unayosema (Kafulila).
“Ndio maana tukasema tufunge mikanda na kuhakikisha bajeti yetu haiwi tegemezi,” alisema.
 
Fedha ambazo Tanzania ilipaswa kupata kupitia MCC awamu ya pili ni Dola milioni 450 (Sh. bilioni) 765.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment