Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, May 17, 2015

Wahusika kashfa ya Escrow na Tokomeza bado wanachunguzwa

Image result for Profesa Sospeter Muhongo


Licha ya kusafishwa na Ikulu, wahusika wa kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow na Operesheni Tokomeza bado wako kwenye hati hati wakiendelea kuchunguzwa kama wana mashtaka ya kujibu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliliambia Bunge jana wakati akijibu hoja zilizoulizwa na wabunge waliochangia hotuba na bajeti ya ofisi yake.

Wakitoa michango yao baadhi ya wabunge walihoji hatua ya kuwasafisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na aliyekuwa waziri wa wizara hiyo, Profesa Sospeter Muhongo na kuwaacha wengine.

Kadhalika walishangazwa kuwaondolea lawama mawaziri waliowajibika, Dk. Emmanuel Nchimbi-Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hamis Kagasheki-Maliasili na Utalii na Shamsi Vuai Nahodha Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa licha ya kwamba Bunge liliwapata na hatia ya kushindwa kusimamia opereshini hiyo na kutaka wawajibike kwani ilisababisha vifo, udhalilishaji, mateso kwa watu na uharibifu wa mali.

Mwingine ambaye alilazimika kujiuzulu katika sakata hilo ni Dk. David Mathayo wa Maendeleo ya Mifugo, japo Bunge halikumuwajibisha. Hata hivyo, Waziri Mkuu hakusema jinsi ya kuwasaidia waathirika wa tokomeza.

Akifafanua, alisema mawaziri hao walionekana hawana hatia kwenye kipengele cha maadili ambacho ndicho kamati ilichotumia kuwachunguza.

Alisema hilo halijamaliza mchakato wa kuwachunguza kwa vile taasisi kama polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) zinaendelea kuchunguza iwapo walifanya jinai.

Alifafanua kuwa vyombo hivyo vinachunguza, kama kuna ushahidi wa kutosha watashtakiwa hata kama tume na kamati ziliwaona hawana lawama.

Aliongeza kuwa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue, kuwa Maswi hakuwa na hatia ilitokana na ripoti ya uchunguzi iliyoandaliwa na kamati ya makatibu wakuu iliofanya uchunguzi huo.

Kwa upande wa Tokomeza taarifa ilitokana na ripoti ya kamati iliyowachunguza na kubaini kuwa hawakuhusika moja kwa moja kwa kuzingatia eneo la maadili.

“Hata hivyo ripoti hiyo haiwaondoi kwenye adhabu ya kuwajibika kisiasa.
Hilo linabakia kama lilivyo.” Alisisitiza.

Alieleza kuwa pamoja na ripoti hizo kutoa taarifa hizo, wale waliopatikana na hatia kwenye kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow wataendelea na mashtaka yao.

“Lakini kubwa zaidi mamlaka ni ya Rais ndiye mwenye kauli ya mwisho juu yao ndiye anayeweza kusema nini kifanyike…” alisema.

Wiki hii baadhi ya wabunge akiwamo, Tundu Lissu, Singida Mashariki (Chadema), James Lembeli, Kahama (CCM), Peter Serukamba, Kigoma Mjini (CCM), walieleza kushangazwa na ripoti za uchunguzi kuwasafisha wahusika.

Walizishangaa ripoti hizo kushindwa kuzungumzia namna ya kuwalipa fidia ndugu ya watu waliokufa, waliojeruhiwa na kupata ulemavu au kuharibiwa mali zao kwenye sakata la tokomeza.

Hata hivyo, walitaka kila aliyehusika asafishwe na kusiwe na upendeleo wa kuwasafisha Profesa Muhongo na Maswi na kuwaacha wengine.

UCHAGUZI
Alisema siku saba za kusajili wapiga kura kwa kila mkoa kutatosha kutokana na idadi ya kutosha ya vifaa vya usajili.

Alisema licha ya kupanga wiki moja zinaweza kuongezeka kama wananchi hawajasajiliwa.

Akizungumzia hofu ya baadhi ya watu waliotimiza miaka 18 umri wa kupiga kura kuachwa alisema, amewasiliana na Tume ya Uchaguzi (NEC) kuhusu makisio ya wapiga kura na kuambiwa idadi yao ni milioni 24.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment