Yadaiwa ni kwa bei ya Sh86 bilioni, baada ya halmashauri kushindwa kulipa kodi.
Dar es Salaam. Jengo la Machinga Complex linatarajiwa kuuzwa kwa wafanyabiashara wa China kwa Sh86 bilioni na Manispaa ya Jiji la Dar es Salaam baada ya kushindwa kulipa kodi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Machinga Comlpex, Gerald Mpangama amesema wamebaini njama za kuuzwa kwa jengo hilo ambalo linasimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema taarifa ambazo walizipata ni kwamba jengo hilo limeshaanza kufanyiwa tathmini na raia wa China ambao wameshakuja na kuangalia mandhari yake.
“Tunajua fika kuna kitu kilichofichika nyuma nacho ni suala zima la uuzwaji wa jengo la wafanyabiashara wadogo wadogo la Machinga Complex kwa wachina, kwani hata agenda namba 7 ya kikao cha bodi kilichopita kilizungumzuia suala la uuzwaji wa jengo hili,” alisema Mpangama.
Mpangama alibainisha kuwa sababu walizoelezwa za kuuzwa kwa soko hilo ni kwamba linajiendeshwa kwa hasara licha ya wafanyabiashara hao kulipa kodi ya vizimba.
Mpangama aliweka wazi kuwa wafanyibiashara hao hawatakubali soko hilo liuzwe na wanajipanga kugoma kupinga uuzaji huo.
Diwani wa Kata ya Upanga, Godwin Mbaga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi na Uendeshaji wa jengo hilo alikana kuhusu taarifa hiyo na kusema kuwa mwenye majibu mazuri ni halmashauri ya jiji kwani wao ndiyo waliokabidhiwa kusimamia na wanaofahamu gharama zote.
Naye Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kebwe alisema hana taarifa za uuzwaji wa jengo hilo na anazisikia kwa waandishi wa habari. “Aliyekupa taarifa hizi mwambie yeye ndiye akupe ukweli wa uuzwaji, ninachojua jengo linadaiwa.”
lakini hapa sina data zozote’’alisema
Jengo la Machinga Complex ambalo limejengwa kwa Fedha za Mkopo kutoka NSSF wa zaidi Bilioni 16 na linatarajiwa kuuzwa kwa Bilioni 86 kwa watu kutoka China.
(1).jpg&container=blogger&gadget=a&rewriteMime=image%2F*)
No comments :
Post a Comment