dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, July 7, 2015

Dk Shein afanya mazungumzo na Balozi mpya wa Japan Ikulu

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana  na   Balozi mpya wa Japan katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Masahau Yoshinda alipofika Ikulu Mjini Unguja leo kujitambulisha kwa Rais,[Picha na Ikulu.]
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na na  Balozi mpya wa Japan katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Masahau Yoshinda alipofika Ikulu Mjini Unguja leo kujitambulisha kwa Rais,[Picha na Ikulu.]



        
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
    Zanzibar                                                       06 Jula, 2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amekutaka na Balozi mpya wa Japan nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshinda na kumueleza kuwa matarajio ya Zanzibar ni kuona ushirikiano kati yake na nchi hiyo unaimarika zaidi katika kipindi chote Balozi huyo atakapokuwa anaiwakilisha nchi yake humu nchini Tanzania.

Dk. Shein alibainisha kuwa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania imekuwa na ushirikiano wa karibu na Japan ambapo matokeo ya ushirikiano huo ni pande mbili hizo kushirikiana katika kutekeleza miradi mbalimbali katika sekta za huduma za jamii, kilimo, mafunzo na nishati.

Katika mnasaba huo, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi aliipongeza Serikali na kuwashukuru wananchi wa Japan kwa misaada yao mbalimbali ambayo imekuwa ikisaidia kuharakisha maendeleo na ustawi wa wananchi wa Zanzibar.

Akitoa mfano wa miradi hiyo, Dk. Shein aliutaja mradi wa uimarishaji wa huduma za maji (awamu ya kwanza na ya pili) katika mji wa Zanzibar ambapo hivi sasa umeongeza kiwango cha upatikanaji maji kufikia asilimia 87.

Miradi mingine ni wa ujenzi wa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji maji wa kekta 2,000 pamoja na msaada wa shilingi bilioni 50 kwa ajili kuimarisha huduma za umeme.

Alifafanua kuwa mradi wa umwagiliaji utakapokamilika utaongeza mavuno ya mpunga hivyo kusaidia katika kufikia lengo la serikali la kujitosheleza kwa chakula hasa mchele na kuongeza kuwa msaada kuimarisha huduma za umeme umesaidia kuondosha kabisa tatizo la umeme kupungua nguvu mara kwa mara.

Katika mazungumzo hayo Dk. Shein alimueleza Balozi Yoshinda kuwa Zanzibar ingependa kuona ushirikiano wake na Japan unapanuka kwa kukaribisha wawekezaji kutoka nchi hiyo kuwekeza Zanzibar katika sekta mbalimbali lakini akatilia mkazo sekta za Uvuvi na Utalii.

Alieleza kuwa sekta hizo mbili zina uwezo wa kutoa mchango mkubwa katika uchumi wa Zanzibar na kubadili haraka ustawi wa wananchi wake endapo itaweza kuvutia uwekezaji mkubwa ambao serikali ndio inaouhimiza.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi alimueleza Balozi huyo kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Japan katika maeneo yote ambayo yana maslahi kwa maendeleo ya Zanzibar na watu wake.

Dk. Shein alimhakikishia Balozi Yoshinda kuwa yeye binafsi na viongozi wa Zanzibar watampa ushirikiano unaopaswa ili aweze kutimiza majukumu yake wakati wote akiwa nchini katika kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi yake.

Kwa upande wake Balozi Yoshinda alisema anafurahi kuona kuwa uhusiano na ushirikiano kati nchi yake na Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla ni nzuri na kwamba zaidi ni wa kuridhisha kwa pande zote mbili.
Alibainisha kuwa nchi yake ingependa kuona ushirikiano wake na Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaendelea kudumu kwa kupanua maeneo mapya ya ushirikiano hasa uwekezaji.

Balozi huyo aliisifu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mafanikio makubwa iliyoyapata katika vita dhidi ya ugonjwa wa malaria na kueleza kuwa hayo ni hatua muhimu katika kustawisha maisha ya wananchi wa Zanzibar.

Balozi Yoshinda alisema ikiwa ni mara yake ya kwanza kufikia Zanzibar anapanga kutembelea kisiwa cha Pemba kuangalia maendeleo ya huko na kuwa amefurahi kuona nchi yake inachangia katika maendeleo na ustawi wa watu Zanzibar.

Alimhakikishia Mheshimiwa Rais wa Zanzibar kuwa Japan itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta mbalimbali za maendeleo pamoja na mafunzo kwa wataalamu wa sekta mbalimbali.

/ZanziNews.

No comments :

Post a Comment