dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, July 30, 2015

Upinzani Zanzibar: Lowassa ataisambaratisha CCM.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa.
Siku moja baada ya Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (pichani), kujiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), viongozi wa vyama kadhaa vya siasa Zanzibar  wamesema uamuzi huo  unaweza kuitikisa CCM.
Mwenyekiti wa ADC, Said Miraji, alisema tukio hilo ni la kihistoria na ni rekodi mpya kiongozi kama huyo ambaye ana ushawishi mkubwa kutoka CCM na kujiunga Chadema.
Alisema uamuzi huo wa Lowassa kung’oka na kwenda chama cha upinzani chenye nguvu kubwa Tanzania Bara, hauwezi kukuacha CCM salama.
Alisema Lowassa sasa amezaliwa upya kisiasa na kama CCM haikuwa makini inaweza kuondoka madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Juma Ali Khatibu, Makamu Mwenyekiti wa Tadea, alisema anaheshimu sana maamuzi ya Lowassa na kuwa upinzani utakuwa mkubwa katika uchaguzi mkuu.
Hata hivyo, alisema vyama vya upinzani vina kazi kubwa ya kuking’oa CCM kutokana na kuwa na imizizi mirefu.
Alisema bunge lijalo la 11 litakuwa na wabunge wengi wa upinzani.
“Katika siasa hakuna adui wala rafiki wa maisha, wale ambao walikuwa wanamponda Lowassa leo hii ndio amekuwa rafiki mkubwa kwao,” alisema Juma.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ali Vuai, alisema Lowassa kuhama CCM hakutakidhoofisha chama tawala na kitaendelea kuwa imara.
“Lowassa na vyama vya upinzani havina ubavu wa kuing’owa CCM kwa sababu CCM ni chama makini kinachokubalika na kina dhamira njema kwa wananchi bila ya kujali dini, rangi wala ukabila,” alisema Vuai.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment