RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitashinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
Alisema kauli inayozungumzwa na wapinzani kwamba chama hicho kimekuwa kikiiba kura katika uchaguzi ni kauli za ghiliba na vitisho ambazo hazipaswi kutolewa na kiongozi aliyebobea.
Rais huyo wa Zanzibar pia alisema hakuna sababu za msingi za kuifanyia mabadiliko Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ikiwamo kuwaondoa watendaji kama anavyotaka Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Dk. Shein ametoa msimamo huo siku moja baada ya mgombea urais wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kumlaumu kuwa ameshindwa kutekeleza ahadi ya kuifanyia mabadiliko ya watendaji tume hiyo kwa miaka mitano tangu aingie madarakani mwaka 2010.
Dk. Shein alisema tangu aingie madarakani hajaona matatizo ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar, na ripoti ya Tume yam waka 2010 haijaeleza kama watendaji wa tume hiyo wana kasoro za utendaji kama inavyolalamikiwa na kambi ya upinzani visiwani Zanzibar.
Dk. Shein aliyasema hayo Mjini Unguja baada ya kuchukua fomu ya kugombea urais visiwani humo jana.
Alisema CCM itashinda kutokana na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi na pia kusimamia ilani yake na kuitekeleza kwa asilimia 90.
/Mtanzania.
No comments :
Post a Comment