Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, August 5, 2015

Magufuli atikisa uchukuaji fomu.

Dk. John Magufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan, wakiwasalimia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam jana.
Mgombe uraiswa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli jana alichukua fomu za kuwania nafasi hiyo huku Mwenyeti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiwaasa wanachama wa chama hicho wasimpuuze adui yeyote katika uchaguzi mkuu mwaka huu na kutamba watafunga magori uwanjani huku wapinzani wakiwatazama.
 
Magufuli alichukua fomu hizo katika ofisi za Tume ya Taifa ya  Uchaguzi (Nec) kwa mbwembwe akiwa kwenye msafara wa magari, pikipiki, matarumbeta na muziki.
 
Akizungumza na wanachama wa CCM jana mchana katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete aliwasihi wanachama wa chama hicho kutodharau adui yeyote watayepambana naye katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
 
Licha ya Rais Kikwete kutofafanua kauli yake hiyo, katika uchaguzi mkuu ujao CCM inatarajia kupambana vikali na mgombea urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa aliyehama Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hivi karibuni.Lowassa alikihama CCM huku akisema kwamba ameamua kufanya hivyo kutokana na kubakwa kwa demokrasia ndani ya chama hicho kikongwe nchini.
 
Kikwete alisema katika uchaguzi wa mwaka huu, chama hicho kitafunga magori uwanjani huku upinzani ukitazama na kwamba kitapata ushindi wa kishindo na hilo hana wasiwasi nalo.
 
Rais Kikwete jana alionekana mwenye furaha muda wote huku akiomba kikundi cha kwaya cha TOT, kimuwekea wimbo wa 'acha waseme CCM kina wenyewe, shangilia ushindi unakuja'.
 
Wakati wimbo huo ukipigwa, Kikwete aliamua kuucheza akiwa jukwaani huku akishangiliwa na wananchi waliokusanyika katika ofisi za CCM.
 
Hata hivyo, Rais Kikwete hakuzungumzia juu ya kuondoka  Lowassa ndani ya CCM, na kwenda kujiunga na Chadema kisha kuteuliwa kugombea urais kupitia umoja huo.
 
Alisema dunia nzima inajua maendeleo mazuri yaliyofikiwa kupitia utawala wake na kwamba katika kampeni watakwenda kuwaeleza wananchi mambo mazuri yaliyofanywa.
 
Alijivunia maendeleo makubwa yaliyopatikana katika utawala wake na kusisitiza kuwa anaondoka madarakani huku akiiacha nchi ikiwa na amani, umoja na mshikamano.
 
Wakati wa kwenda kuchukua fomu ya kugombea urais, Dk. Magufuli jana aliambatana na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), huku wakisindikizwa na viongozi mbalimbali waandamizi wa CCM.
 
Wengine ni wajumbe wa kamati kuu za CCM, baadhi ya mawaziri, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecki Sadiki.
 
Tukio hilo lilisababisha shughuli za mbalimbali za wananchi kusimama kwa muda kupisha msafara huo kupita wakati ukitokea Nec kuelekea ofisi za CCM kabla ya kuhutubiwa na wagombea na viongozi wa chama hicho.
 
Mgombea huyo alichukua fomu jana mchana katika ofisi ya Nec  kisha msafara wake ambao ulifunga barabara za Bibi Titi Mohammed, Morogoro  na Ohio, ulirudi ofisi ndogo za CCM zilizopo Mtaa wa Lumumba ambako aliwahutubia wanachama na wapenzi wa chama hicho.
 
KINANA
Akimkaribisha Rais Kikwete kuwatuhutubia wanachama hao na wapenzi wa CCM, Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdurlahman Kinana, alitoa maneno makali huku akidai wanachama waliohamia upinzani kuwa ni makapi.
 
Kinana alidai  CCM hakiwezi kupambana na makapi katika uchaguzi huo wa madiwani, wabunge na rais huku akisisitiza kuwa ushindi ni lazima upatikane kwa chama hicho Oktoba 25, mwaka huu.
 
MAGUFULI
Kwa upande wake , Dk. Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, alisema shida zote za Watanzania anazifahamu na mategemeo yao anayafahamu na kuendelea kuwaahidi kwamba hawaangusha wakimpa nafasi ya kuwa rais wa serikali ya awamu ya tano.
 
Alisema serikali ya awamu ya nne imefanya mambo mengi yakiwamo ya ujenzi wa barabara ambazo pia wapinzani wanazitumia kupita, hivyo akishinda,  ataziendeleza.
 
"Mnitume nitakuwa mtumishi wenu mzuri kwa kuwa shida za Watanzania nazijua na sitawaangusha hata kidogo,'' alisema huku akishangiliwa.
 
Alisema kila akiangalia haoni mtu wa kushindana naye na kumshinda katika uchaguzi huo utakaovishirisha vyama vingi vya siasa.
 
"Mmepoteza nguvu zenu nyingi, muda wenu mwingi, mmetembea umbali mrefu kuja kunisikiliza, napenda niwahakikishie kwamba CCM itashinda," alisema.
 
Dk. Magufuli jana aligeuka kivutio baada ya kutoa salaam kwa ufasaha kwa kutumia lugha za kisukuma, kimasai, kichaga, kihehe, kihaya na  kinyakyusa.
 
SAMIA
Naye mgombea mwenza, Samia, alimpiga kijembe aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Segerea, Dk. Makongoro Mahanga aliyejiunga na Chadema wiki hii.
 
Wengine waliojiunga na Chadema ni pamoja na Mbunge wa Kahama, James Lembeli, Godluck Ole Madeye (Arumeru Mashariki), Ester Bulaya (Viti Maalum) na aliyekuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM wa Mikoa na Mkoa wa Singida, Mgana Msindai.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment