AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, August 2, 2015

Mgeja: Lowassa kuhama CCM si jambo dogo

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, amesema kitendo cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kuhama chama hicho na kujiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) si jambo dogo na la kutolea majibu mepesi.

Akizungumza na NIPASHE Jumapili jana, Mgeja alisema kilichotokea Dodoma bado Lowassa anakitafakari kama kiongozi na mwanasiasa kutokana na ukubwa wa jambo lenyewe, hivyo hata kujiondoa kwake na kujiunga Chadema lazima kusichukuliwe jambo dogo.

Mgeja alitoa maoni hayo baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu akiwa mdau wa karibu na Lowassa wakati wa kampeni za kusaka wadhamini wa urais kupitia tiketi ya CCM kabla hajaenguliwa na kamati kuu ya chama hicho.

Alisema ingawa ni uamuzi binafsi pamoja na familia yake, lakini ni jambo kubwa la kiongozi wa juu kujiunga na upinzani ambalo mtu yeyote anashindwa kulitolea majibu kamili.

“Uamuzi mgumu na si jambo dogo, tena ni zito ambalo halihitaji majibu mepesi kuhusu kuondoka kwa Lowassa CCM na kujiunga Chadema...kwangu bado nayatafakari yale yaliyotokea Dodoma kwa sababu waziri huyo aliwekeza sana ndani ya chama kilichomlea na kumkuza tangu akiwa kijana,” alisema Mgeja.

Mgeja ambaye pia ni mwenyekiti wa taasisi ya Mzalendo Foundation, alisema kila mmoja aliguswa kuondoka kwa Lowassa CCM na kwenda Chadema ambcho ni chama kikuu cha upinzani nchini kwa sasa.

Hata hivyo, alisema mambo yaliyotokea katika mkutano wa kuteua mtu atakayewania kiti cha Rais kwa tiketi ya CCM mkoani Dodoma, yanatakiwa waachiwe wanaCCM wenyewe wayazungumze katika vikao vyao vya ndani kuliko kuzungumzia nje.

“Tulimzoeya sana, tumesikitika na wengi tunaamini tumemkosa ndani ya chama ila kwangu bado mwanachama na kiongozi wa CCM bali tuendelee kutafakari yaliyotokea huko na tuyajadili ndani ya vikao,” alisema.

Licha ya Lowassa kuwa kiongozi wa juu kujiunga na upinzani, lakini aliyekuwa waziri kiongozi wa serikali ya Maopinduzi ya Zanzibar, Seis Shariff Hamad, alilazimishwa kujiuzulu na baadaye kujiunga chama cha wananchi (Cuf).

Mwingine ni Augustino Mrema aliamua kuachana na CCM akiwa Naibu Waziri Mkuu (cheo alichopewa kinyume na katiba) huku akiwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana na kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment