Aidha, CCM imeambulia ushindi katika kata tano kati ya 20 zilizopo jimboni hapa, hali ambayo inayoonyesha wazi kwamba Halmashauri ya Wilaya ya Monduli itaongozwa na mwenyekiti kutoka Chadema.
Baada ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Monduli, Ephraim Olenguyaine, kumtangaza Kalanga kuwa mbunge mteule wa jimbo hilo, mamia ya wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ukumbi wa Halmashauri ya Monduli, ulilipuka kwa shamra shamra na vifijo.
Wakati matokeo hayo yakitangazwa jana saa 7: 00 mchana. Namelok ambaye alikuwa mbunge wa Viti Maalum wa CCM kutoka Mkoa wa Arusha, hakuwapo ukumbini wakati wa kutangazwa kwa matokeo, ingawa majira ya asubuhi alishiriki majumuisho ya kura kutoka kata zote 20.Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro, alikuwapo katika ukumbi huo uliofurika wanachama wa Chadema na washabiki wao. Mawakala wa Namelok nao pia walikuwapo.
Akitangaza matokeo ya mgombea mwingine kutoka ACT - Wazalendo, Navaya Ndaskoi, Olenguyaine alisema kuwa alipata kura 367.
Akizungumza na wapiga kura nje ya ukumbi huo, mbunge mteule Kalanga, aliwashukuru kwa kura nyingi walizompa na akaahidi kufanya kazi ya kuwatumikia.
“Nitafanya kazi ya kuwatumikia kuwaletea maendeleo, naombeni ushirikiano wenu ili tufanikiwe katika azma yetu.
“Nawashukuru wote na hata waliokuwa wagombea wenzangu. Nawaomba tuungane pamoja kuangalia maslahi ya wana-Monduli,” alisema.
Kwa upande wa matokeo ya kata, CCM imeshinda katika kata za Selela, Engaruka, Lashaine, Lemooti na Mfereji, wakati Chadema imeshinda kata za Naalarami, Engutoto, Esilalei, Lepurko na Lolkisale.
Kata zingine ni Majengo, Makuyuni, Meserani, Migungani, Moita, Monduli Juu, Monduli Mjini, Mswakini, Mto wa Mbu na Sepeko.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment