Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 9, 2015

Dk. Shein aahidi neema kwa wafanyabiashara!

IMG_5897Na Esther Mbussi, Zanzibar
MGOMBEA urais wa Zanzibar, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Ali Mohamed Shein amesema maendeleo kwa wafanyabiashara wadogo visiwani humo ni lazima.
Kutokana na hali hiyo, ameahidi kuwajengea eneo la maonyesho ya biashara ili kuwavutia wafanyabiashara wa nje.
Akizungumza katika viwanja vya Urafiki, Jimbo la Sahurimoyo mjini Unguja juzi, Dk. Shein alisema mradi huo licha ya kuwavutia wafanyabiashara, utawasaidia kutangaza biashara zao.
“Wafanyabiashara wadogowadogo ndiyo wanaofanya biashara wengi, hatuwezi kuwatupa au kuwanyanyasa, tuwajengee uwezo madhubuti, tayari Serikali imeanza mazungumzo na watu mbalimbali kuhakikisha wanatimiza azma ya ujenzi wa eneo hilo.
“Nitahakikisha ujenzi huu,unakamilika mapema kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali yakiwamo mifuko ya hifadhi ya jamii na benki zetu,” alisema.
Alisema  miaka mitano ijayo, atazidisha ushirikiano na sekta binafsi ili kuwasaidia wafanyabiashara wadogo wadogo.
/Mtanzania.

No comments :

Post a Comment